Katika
kuelekea Maadhimisho ya Miaka 61 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi
Huru za Afrika Mabalozi zaidi ya 62 na Wanadiplomasia wanatarajia
kushiriki Mbio za Afrika Marathon za Kilometa 5 hadi15 zinazotarajia
kufanyika Mei18 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na wanahabari jijini humo Mkurugenzi wa Idara ya Afrika - Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ally Bujiku
amesema kuwa mbio hizo zitafanyika kuelekea kuadhimisha miaka 61ya
maadhimisho ya umoja wa nchi hizo na kwamba zina lengo la kukuza
Diplomasia katika sekta ya michezo.
"Michezo
ni biashara,ni ajira ni kazi pia ni Diplomasia,tumechagua riadha
kwasababu kila mtu anaweza kushiriki" amesema Balozi Bujiku.
Amebainisha kuwa mbio
hizo zitaanzia katika Daraja la Tanzanite, Mtaa wa Barrack Obama hadi
Masaki na kwamba fedha zitakazopatikana zitapelekwa Shule za Wanafunzi
wenye mahitaji maalum.
Amesisistiza
kuwa mabalozi watatoa misaada katika shule hizo huku akiwahimiza
wananchi kushiriki kwa wingi kufanikisha maadhimisho hayo.
Ameongeza
kuwa baada ya Marathon Mei 20 mwaka huu washiriki wote wa mbio za
maadhimisho hayo watashiriki chakula cha jioni cha pamoja katika Hoteli
ya Serena.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wizara hiyo, Balozi Mindi Kasiga amesema mbio hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa wanariadha wakongwe akiwemo Juma Ikangaa.
Balozi Mindi amefafanua kuwa shule
zitakazopata misaada itakayotolewa kuelekea maadhimisho hayo ni Pugu,
Uhuru Mchanganyiko pamoja na Shule ya Sekondari Jangwani.
Pia amesema Mei 25, 2024 ambapo ndio kilele cha maadhimisho hayo Tanzania italipokea Baraza la Amani na Usalama
Nae,
Balozi wa Kenya Nchini Tanzania, Isaac Njenga amesema kuwa atashiriki
mbio hizo kwani zina umuhimu mkubwa kudumisha amani, umoja na mshikamano
wa nchi za Afrika
Balozi
wa Somalia Nchini Tanzania, Yassini Ally khali amesema yupo tayari
kukimbia kilometa 15 zitakazoanzia Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere hadi
Masaki.
No comments:
Post a Comment