NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti amefanya kikao kazi na wataalam wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyi pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya kwa ajili ya kujadili maendeleo ya Mradi wa viwanja vya Uwekezaji wa Viwanda.
Mkuu wa Wilaya hiyo pia katika kikao hicho ameweza kuongozana na Viongozi mbali mbali wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na Timu ya Watalaam na kupata fursa ya kutembelea eneo la Mradi wa upangaji wa Upimaji wa Eneo la Viwanda lililopo Visegese kata ya Kazimzumbwi.
Mhe.Magoti alisema kwamba mradi wa Upangaji wa upimaji ulibuniwa kwa ajili ya kutenga viwanja kwa ajili ya Viwanda na Maeneo mbali mbali ya Makazi ya watu.
Magoti alifafanua kuwa utekelezaji wa Mradi huo ulianza kutekelezwa.mnamo mwaka 2014 na kufanikiwa kuzalisha Viwanja 291 hivyo eneo hilo litakuwa Maalum kwa ajili ya Viwanda vya aina mbali mbali.
"Utekelezaji wa Mradi huu ulifanyika kwa ubia kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na Wananchi wenye Maeneo katika Eneo lililopendekezwa kwa lengo la uwelezaji huo,"alisema Mhe.Magoti
Mkuu huyo alieleza kuwa muda si Mrefu Wananchi wote wenye nia yakutaka kuwekeza nakujenga Viwanda Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa pwani karibuni sana sana.Huduma za Maji zipo na barabara tupo mbioni kuzishughulikia ili kupanua wigo wa usafirishaji.
Pia alifafanua kwamba Mhe. Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan anapenda kuona Wananchi wake wanapata kipato kikubwa na kuinua uchumi wa kimaendeleo yenye kuleta mabadiliko na kuboresha maisha yao kwa ujumla.
June 20, 2024
Home
Unlabelled
DC KISARAWE AUNGANA NA WATAALAM KUJIONEA MWENENDO MRADI WA VISEGESE
DC KISARAWE AUNGANA NA WATAALAM KUJIONEA MWENENDO MRADI WA VISEGESE
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment