HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 01, 2024

FEI TOTO AWATAHADHARISHA WANACHI FAINALI CRDB FC

Na John Richard Marwa

Kiungo nyota wa Azam FC Feisal Salum Fei Toto amesema licha ya heshima kubwa wanayowapatia wapinzani wao Yanga SC kuelekea mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB Federation Cup hapo kesho wako tayari kunyakua taji hilo.

Fei Toto amesema hayo mapema leo katika mazungumzo na waandishi wa Habari kuelekea mchezo huo wa Fainali utakaopigwa katika Dimba la New Amani Complex Zanzibar.
 

"Kwa upande wa wachezaji tumejipanga vizuri, tuko tayari kikubwa sisi tutafuata maelekezo ya benchi la ufundi.

Tunawaheshimu sana Yanga, wana wachezaji wazuri tunafahamu hilo hivyo tunawaheshimu sana Yanga ila na wao waje kwa kutuheshimu kwa sababu wakifanya makosa tutawaadhibu.

"Tulishapoteza Fainali ya kwanza dhidi yao na hii hatuwezi kukubali kikubwa tutafuata maelekezo ya mwalimu. Nafurahi Fainali hii inachezwa hapa nyumbani na niko tayali kwa huu mchezo." amesema Feisal Salum.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Azam FC Bruno Ferry amesema "Tunafuraha kwa sababu tunaenda kucheza fainali na bingwa wa msimu huu. Nawapongeza Yanga kwa ubingwa.

"Kwa kesho tumejiandaa vema na tunafahamu msimu huu wamepoteza michezo mitatu na moja wapo ni dhidi yetu hivyo tumejiandaa kwa ajili ya kuhakikisha tunapata tunachostahili kwenye hii Fainali." amesema Bruno Ferry.



No comments:

Post a Comment

Pages