NA VICTOR MASANGU, KILIMANJARO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi Mzee Francis Koka kilichotokea Moshi, Kilimanjaro.
Akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Mhe Rais Mwakilishi wake Felister Mndeme alisema ameagizwa na Rais kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuungana na familia ya Mbunge Koka kwa ajili ya kuweza kutoa pole na kuungana katika mazishi.
"Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameniagiza kuja hapa Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kutoa pole kwa Mhe Koka na kwamba yupo pamoja na familia katika kipindi hiki cha maombolezo,"alisema Mdeme kwa niaba ya Rais.
Mdeme alisema kwamba Rais Dkt. Samia alitamani kujumuika katika Msiba huo lakini ameshindwa kufika kutokana na kuwepo na majukumu mengine.
Mwakilishi huyo wa Rais alibainisha kwamba Mhe Rais anatambua Mchango wa Mzee Francis Koka (WW1 Veteran) na kwamba ni vyema kuenzi historia ya kipekee iliyoachwa na Marehemu ambaye ni Baba Mzazi wa Mhe Koka Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini.
Mazishi ya baba yake mzazi na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka yamefanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Mkolowony Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,mawaziri wabunge viongozi wa vyama vya siasa,madiwani,taasisi binafsi pamoja na wananchi.
June 01, 2024
Home
Unlabelled
RAIS SAMIA ATUMA POLE KWA MSIBA WA BABA YAKE MZAZI WA MBUNGE KOKA
RAIS SAMIA ATUMA POLE KWA MSIBA WA BABA YAKE MZAZI WA MBUNGE KOKA
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment