Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo, Hassan Bomboko, akitoa hotuba yake wakati wa kufungua rasmi kituo cha kutoa elimu ya kujiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF) iliyokwenda
sambamba na upimaji wa afya bure katika kituo cha mabasi cha kimataifa cha Magufuli jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni,
Dk. Raphael Mallaba. (Na Mpiga Picha Wetu).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kinondoni, Dk. Raphael Mallaba, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha kutoa elimu ya kujiunga na Mfuko huo iliyokwenda
sambamba na upimaji wa afya bure katika kituo cha mabasi cha kimataifa cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
Serikali
imesema upo umuhimu wa kuuongezea nguvu Mfuko wa Afya Bima ya Afya wa
NHIF ili uweze kufikisha elimu kwa umma juu ya faida za kuwa na bima ya
afya kwa maslahi mapana ya mtanzania mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe; Hassan Bomboko wakati wa ufunguzi wa kituo cha kutoa elimu katika kituo cha mabasi
cha kimataifa Mgafuli kilichopo mbezi jijini Dar es Salaam.
"Sisi kama serikali tumeona upo umuhimu wa kuwapa nguvu NHIF
kufikisha elimu kwa umma na nitumie hadhara hii kutoa maelekezo kwa
watendaji wa kata na mitaa, kwamba kwenye mikutano yote ya hadhara wawape
elimu wananchi juu ya umuhimu wa mfuko wa NHIF kwa wananchi wetu,
"Iwe
ajenda, na kaimu afisa tawala uko hapa, magavana wote muifanye hii kazi
ya kuhakikisha katika ziara zenu mikutano yenu ya kuwaelewesha wananchi
kwamba dunia ya sasa inakuhitaji kuwa na bima ya afya ili uweze kupata
huduma kirahisi pasi na kulazimika kutumia pesa ambayo hukuwa umepanga
kuitumia .
Japo la pili wananchi tuwe na
utamaduni wa kupima afya zetu, leo nimekuta hapa zoezi linaendelea na ni
zoezi zuri lialofanywa na wenzetu wa Kairuki nawapongezeni sana,
wananchi wetu wamepata huduma hapa na ni huduma ambayo wameipata bila
malipo yoyote kwaiyo tunawashukuruni na mfikishe shukrani zetu kwa
wakurugenzi na nyie ambao mko hapa kuendesha zoezi hili.
Ilani
ya Chama cha Mapinduzi imeelekeza kwamba wananchi wapate elimu juu ya
namna ya kujiunga katika bima ya afya, mzifikie na shule zetu za msingi na sekondari muwape
elimu wanafunzi na wazazi juu ya faida ya kujiunga na mifuko ya bima ya
afya."amesema Bomboko
Niwapongeze sana NHIF kwa kutoa huduma na
kuwafikia wananchi wengi. Wananchi wamekuwa wakipatiwa huduma mbalimbali
jambo la msingi ambalo limekuekuwa likiendelea ni NHIC kuona ipo haja
Serikali kuwa na kituo hapa katika wilaya yetu ya ubungo.
Toka
kituo hiki kimefunguliwa kimekuwa na mafanikio makubwa sana nje na
utaratibu wa kawaida kimewafikia watu wengi sana na kuwapa elimu na hii
elimu ndiyo imewaondoa wasiwasi wananchi kwamba tunatoa hela lakini
yawezekana ni siumwe mimi nikakaa muda mrefu na hela yangu ikaenda bura,
lakini leo wamejua umuhimu wa jambo hili.
Amewataka
wananchi kutambua kuwa sio lazima hadi uumwe ndio uende hospitali, bali
kila mwananchi anaowajibu wa kwenda hospitali kuangalia afya yako na
kuweza kujua hali yako kuliko kusubiri kuugua ndio unakwenda hospitali
kwani itakusaidia kujua nini ufanye ili afya yako iendeleeee kuwa
bora"amesema Bomboko.
"Wananchi
wengi walikuwa wanakuja maofisini kwa ajili ya kupima afya zao na
changamoto ya wanaokuja maofisini wengi wanakuwa ni wagonjwa. hivyo kama
taasisi tumekuwa na mikakati ya kuwafuata huko waliko hapa ni sehemu
moja wapo tu lakini tunatembelea kila maeneo ambayo yana makundi ya
wananchi ili tuwape elimu na wananchi wanapojiunga inarahisha kuwafikia
kwa kiasi kikubwa zaidi. Hivyo muamko umeendelea kuwepo ndio maana hapa
tulipo leo mtashuhudia wananchi wakijaza fomu na kupata bima zao."
amesema Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni, Dk. Raphael Mallaba.
No comments:
Post a Comment