HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 13, 2024

TRENI YA UMEME KUANZA SAFARI YAKE KESHO

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limezindua  kampeni ya uelewa kuhusu kuanza kwa  huduma za usafiri wa Treni katika kiwango Cha kimataifa (SGR) zitakazoanza mwisho wa mwezi wa Julai kutoka Dar es Salaam-Dodoma ambapo tayari shirika limechukua hatua kadhaa ikiwemo kuanza safari zake tarehe mwezi Juni14  mwaka huu.



Hayo yamebainishwa leo Juni 12, 2024  Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa katika hafla ya Uzinduzi wa kampeni hiyo ya uelewa kuhusu kuanza kwa huduma za usafiri wa Treni  ya umeme SGR  yenye  kiwango cha kimataifa  huku furaha kuu ya kuimba kaulimbiu isemayo 'Twende tukapande Treni yetu, tuitunze, tuithamini'.


"Shirika litaanza kutoa huduma za awali za usafiri wa Treni katika Reli ya kiwango Cha kimataifa (SGR) kuanzia Dar es Salaam hadi  Morogoro ifikapo tarehe 14 Juni 2024, hii ikiwa  ni sehemu ya kuendelea kujifunza  teknolojia hiyo mpya nchini na kujiridhisha  mifumo mbalimbali ya uendeshaji huduma za usafiri wa Treni kabla ya kuanza rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam - Dodoma ifikapo tarehe 25 Juali 2024"amesema Mkurugenzi

Wananchi wamesisitizwa kuendelea  kushirikiana kutunza miundombinu ya Reli hiyo kwani ni Mali ya watanzania wote  imejengwa kwa fedha za walipakodi wa kuanza kwa   kutumia huduma hiyo ya usafiri itasaidia  kuongeza pato la Taifa.

Hata hivyo wanaotarajia kutumia usafiri huo watahakikishiwa ulinzi na kutosha kuanzia  abiria na mizigo kwa ujumla.

"Jambo hili ni muhimu sana ni  usalama wa Reli yetu,  usalama wa abiria na mizigo, kwani  kutakuwa na CCTV Camera tutakua na wataalamu  watu ambao watakuwa wanaangalia kila kinachoendelea kwenye treni yetu kwa masaa 24, pia uwepo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama a maaskari ndani ya  Treni ambao watasafiri nasi mwanzo hadi mwisho"

"Kwenye miundombinu, pamoja na kufanya doria, stesheni zetu zote zinavituo vya polisi na tunaimani kuwa kutakua na utaratibu wa kuwepo na maaskari huko njiani, pia Askari watafanya doria, tutakua na walinzi watakuwa wanafanya kazi masaa 24"

Sambamba na abiria wanaweza kukata tiketi kwa njia ya mtandao au kupitia madirisha ya kukatia tiketi ndani ya stesheni kwa njia ya mtandao kwani abiria atatakiwa kukata tiketi wiki Moja au siku 3 kabla ya safari ili kuepukana na msongamano.

Kuhusu nauli Kadogosa amesema tayari LATRA wameshatangaza nauli na hivyo wateja wawe tayari kwa safari na gharama iliyowekwa ni rafiki na wananchi mtu yeyote atamudu

"LATRA wametangaza nauli za daraja la kawaida, lakini tutakua na Treni za aina tatu Tereni ya kawaida itakayosimama Kila sehemu, tutakua na Treni za Moja kwa moja (Express) na Treni mchongoko"

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu wa Benki ya Biashara (TCB) Adam Mihayo amesema katika safari hizo za Reli ya SGR, TCB wameshirikiana na TRC katika kukusanya mapato katika vituo vya kukatia tiketi.

Pia Mihayo amesema Benki ya TCB  wameshirikiana na TRC kwa kufanikisha kuleta vichwa vya Treni na mabehewa kutoka Ujerumani.

"Ushirikiano wetu na Reli ya Tanzania unaakisi dhamira yetu ya pamoja ya kuelewa mahitaji ya watanzania na kuchangia katika ukuaji wa amaendeleo ya kiuchumi na mafanikio ya Taifa letu"

"TCB tutaendelea kushirikiana na shirika la Reli Tanzania ili kuhakikisha matarajio ya Mhe. Rais katika mradi huu yanaweza kutimia" Alisisitiza

No comments:

Post a Comment

Pages