Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam
Viongozi wa Dini nchini wamezitaka Mamlaka za serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter Kwa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga).
Akizungumza na waandishi wa Habari leo juni 11, 2024 Jijini Dar Es Salaam Alhaj Dkt Abdul Suleiman amesema kwamba vitendo vya ushoga vimepigwa vita hata katika maandiko ya dini,hivyo vitendo hivyo havikubaliki na vinapaswa kulaaniwa.
Dkt Sule amesema kwamba kufuatia mtandao wa X (Twitter)kuruhusu kuchapisha maudhui yanayohamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji Mamlaka zinazohusiana na mawasiliano zinatakiwa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ikiwemo kuufungia kabisa mtandao huo.
Kwa upande wake Askofu na Katibu mkuu wa Kanisa la Methodox Tanzania Allen Siso amesema katika vitabu vya dini vyote havikubaliani na ndoa za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,hata wanawake wakabadili matumizi ya asili Kwa matumizi yasiyo ya asili,na wanaume nao vivyo hivyo'.
Kwa upande wake Sheikh Hilal KIPOZEO amesema amesema mtandao wa X unabidi kufungiwa haraka iwezekanavyo kwani ni vyema kutengenezwa Sheria Kali ya Kudhibiti mapenzi ya jinsia moja na usagaji ili kusaidia kizazi kijacho kisiharibike.
"Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka hivyo Mara moja mtandao wa X Ufungiwe"amesema
Naye mwakilishi wa walimu ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Gongolamboto,Munira Njau amesema kuwa wazazi wamekuwa na tabia za kuwaachia watoto wao wachezee simu zao Hali iliyopelekea watoto kuingia kwenye mitandao hiyo na Kujifunza tabia mbaya siku Hadi siku na hatimaye kuzipeleka mashuleni.
"sisi walimu tunashinda na watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni,na tunakutana na wanafunzi ambao tayari Wana viashiria vya tatizo hilo na tunapowahoji wanasema wamekuwa wakisema vimeanzia majumbani na wengine kupitia simu za wazazi wao,hivyo suala hili tuungane wote kusaidia watoto.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida amewaomba vijana wa chama hicho kukemea juu ya matumizi ya mtandao wa Twitter maarufu kama X nchini Tanzania kutokana na kubadilika kwa maudhui ya mtandao huo
Kawaida amesema kuwa hivi karibuni wamepokea taarifa ya kushtua kutokana na mtandao huo kubadilisha maudhui yake na kuanza kuruhusu kutumika kwa picha za ngono maarufu kama ponogroph amewasisitiza walezi na wasimamizi wa maadili ya malezi ya vijana na watoto sio jambo jema kuanza
"Kwanza hata jina lenyewe tu linalotumika limekua na maudhui yanayoendana na masuala ya ponograph, watoto wengi wanatumia simu na wanaingia kwenye mitandao, hivyo sio vizuri kutimika nchini kwetu"amesema Kawaida.
Aidha amesema wao hawana shida na mtandao huo ikiwa wataondoa maudhui yake basi uendelee kutumika ila kama haiwezekeni basi vyema serikali ikaufungia kutokana na kuzalisha maadili yasiofaa
No comments:
Post a Comment