Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Said Shaibu Mussa ameipongeza Benki ya CRDB kwa uamuzi wenu wa
kufanya CRDB Bank Marathon katika nchi tatu kwa maana ya Tanzania,
Burundi na DRC.Balozi Mussa amesema uamuzi huo unaenda sambamba
na jititihda zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi na kuboresha
mahusiano ya kidiplomasia na jirani zetu.
“Hivyo tunapoona
taasisi binafsi kama Benki ya CRDB mkipita katika njia hizo hizo kwa
kutoishia kukuza biashara zenu nje ya mipaka bali kuangalia namna gani
mnaweza kugusa maisha ya watu katika nchi hizo, tunapata faraja na kuona
somo la Dkt. Samia limeeleweka vyema na linatekelezwa kwa vitendo.
Hongereni sana,” awesema Balozi Mussa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela amesema upanuzi wa CRDB
Bank marathon katika nchi za DRC na Burundi unenda sambamba na malengo
ya benki ya kujitanua kikanda na kuchochea maendeleo barani Afrika.
Nsekela
amesema, Benki ya CRDB imejipanga kikamilifu kusaidia kuweka mazingira
wezeshi na kuwawezesha Wananchi katika nchi inapotoa huduma kunufaika na
fursa malengo ya Afrika Tuitakayo “The Africa We Want” 2063.
Nsekela
amesema mafanikio ambayo Benki ya CRDB imeyapata katika nchi za DRC na
Burundi yanatokana na mahusiano mazuri baina ya Tanzania na nchi hizo
yakichagizwa na uongozi mahiri wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi
Evarist Ndayishimye, na Rais wa DRC Congo chini ya Mhe. Rais Félix
Tshisekedi.
Katika
utekelezaji wa mpango wake wa uwezeshaji kwa vijana kupitia CRDB Bank
Marathon, Benki ya CRDB kupitia Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation
imekabidhi msaada wa fedha kwa timu ya Taifa ya Olympic kushiriki katika
Mashindano ya Olympic yatakayofanyika Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 26
Julai hadi 11 Agosti 2024, na leo hii tutawakabidhi hundi ya ufadhili.
Akikabidhi
mfano wa hundi kwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Riaadha Tanzania, William Kallagjhe, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela
amesema uwezeshaji wa timu hiyo ya Taifa ya Olympic kwa vijana
wanaokwenda kushiriki utailetea Taifa heshima, bali pia itawaweka katika
ramani ya kimataifa, ikitoa njia ya mafanikio kwa wao binafsi, familia
zao na jamii kwa ujumla.
Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Said Shaibu Mussa, Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Mhe.
Leontine Nzeyimana, Mwakilishi wa Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) nchini, Patrice Tshekoya na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB
Bank Group, Abdulmajid Nsekela wakikabidhi bendera za Tanzania, Burundi,
na DRC kwa Jeshi la Kusambaza Tabasamu (JLKT) la CRDB Bank Marathon
kama ishara ya kulipa idhini jeshi hilo kusambaza tabasamu katika nchi
hizo.
Malengo msimu wa tano wa CRDB Bank Marathon ni kusajili
wanajeshi wa kusambaza tabasamu (washiriki) zaidi ya 8,000 na kukusanya
zaidi ya shilingi bilioni 2. Katika msimu huu, CRDB Bank Marathon
inatarajia kuanzia jijini Lubumbashi nchini DRC Agosti 4 kisha
tutaelekea jijini Bunjumbura nchini Burundi Agosti 11 kabla ya kurudi
hapa Dar es Salaam Agosti 18.
Balozi wa
Burundi nchini Tanzania, Mhe. Leontine Nzeyimana ameipongeza Benki ya
CRDB kwa kuanzisha CRDB Bank Marathon nchini humo akisema mbio hizo
zitakwenda kusaidia kujenga utamaduni kwa wananchi kujitoa kwa ajili ya
kusaidia wenye uhitaji, pamoja na kuchangia maendeleo katika sekta za
msingi kama afya.
Balozi Nzeyimana amesema kutokana na umaarufu
wa CRDB Bank Marathon kimataifa anategemea kuona mbio hizo kusaidia
kuitangaza nchi ya Burundi kote duniani. Balozi huyo ametoa rai kwa watu
wa Burundi kujisajili kushiriki mbio hizo huku akiwakaribisha washiriki
kutoka Tanzania na nchi nyengine kwenda kushiriki katika mbio zitakazo
fanyika tarehe 11 Agosti 2024.
Akizungumzia mchango wa Benki ya
CRDB katika uchumi wa nchi hiyo, Balozi Nzeyimana ameishukuru Benki kwa
mchango wake katika kusaidia kukuza ujumuishi wa kifedha na kiuchumi
nchini Burundi, huku akiitaja kama moja ya mshirika wa kimakakti wa
Serikali ya nchi hiyo. Pia alitumia fursa hiyo kuipongeza Benki ya CRDB
kwa kuwa benki kiongozi kwa faida ikiwa ni miaka 12 tu toka kuiangia
nchini humo.
Mwakilishi wa
Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) nchini, Patrice
Tshekoya amesifu jitihada za Benki ya CRDB katika kusaidia kutatua
changamoto zinazoikabili jamii. Balozi huyo amesema licha ya muda mfupi
toka kuingia kwa Benki nchini DRC imeonyesha mfano ambao unapaswa kuigwa
na taasisi nyingi wa kujielekeza katika kusaidia changamoto
zinazoikabili jamii.
Balozi Masala ameihakikishia Benki ya CRDB
uungwaji mkono kutoka kwa Serikali pamoja na WaCongo wote katika mbio
hizo akisema ni utamaduni mpya ambao utakwenda kusaidia watu kuwa na
mtindo bora wa maisha, pamoja na kujenga uzalendo wa kujitolea kwa ajili
ya jamii, na Taifa kwa jumla.
Balozi huyo pia alitoa rai kwa
watu wa Congo kujisajili kushiriki mbio hizo huku akiwakaribisha
washiriki kutoka Tanzania na nchi nyengine kwenda kushiriki katika mbio
zitakazo fanyika tarehe 1
Malengo
ya msimu wa tano wa CRDB Bank Marathon ni kusajili wanajeshi wa kusambaza
tabasamu (washiriki) zaidi ya 8,000 na kukusanya zaidi ya shilingi
bilioni 2. Katika msimu huu, CRDB Bank Marathon inatarajia kuanzia
jijini Lubumbashi nchini DRC Agosti 4 kisha tutaelekea jijini Bunjumbura
nchini Burundi Agosti 11 kabla ya kurudi hapa Dar es Salaam Agosti 18.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB Bank Foundation ambaye ndiye Kamanda wa Jeshi la
Kusambaza Tabasamu (JLKT) la CRDB Bank Marathon amesema mbali na makundi
ambayo yamekuwa yakinufaika na mbio hizo mwaka huu katika kuendeleza
azma yetu ya uwezeshaji kwa vijana sehemu ya fedha zitakazokusanywa
zitakwenda kusaidia jitihada za kuwajengea uwezo vijana nchini (capacity
building).
Katika
ripoti iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation
ambaye ndiye Kamanda wa Jeshi la Kusambaza Tabasamu (JLKT) la CRDB Bank
Marathon aliyoiwasilisha wakati wa uzinduzi wa msimu wa tano ambapo mbio
zetu zinavuka mipaka hadi DRC na Burundi amesema;
Katika misimu
minne iliyopita CRDB Bank Marathon imekusanya Shilingi bilioni 2.7
ambazo zilielekezwa katika kusaidia upasuaji kwa watoto zaidi 300 wenye
maradhi ya moyo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), wakinamama
wenye ujauzito hatarishi zaidi 150 Hospitali ya CCBRT, Ujenzi wa Kituo
cha Mawasiliano Taasisi ya Kansa ya Ocean Road (ORCI), ujenzi wa Kituo
cha Afya ya Mama na Mtoto Zanzibar, na kampeni ya utunzaji mazingira ya
‘Pendezesha Tanzania’.
No comments:
Post a Comment