HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2024

MALAIKA WA SHARI KWENYE KICHWA CHA MIGUEL GAMOND

Hieronimus Godfrey
.
Msimu huu itakuwa ni vita ya wenyewe kwa wenyewe, hakuna mwenye hati miliki ya jezi pale jangwani, kikosi hakipangiki, ubora umetawala kila mahali.
.
Leo kwa mara ya kwanza malaika wa shari atatembelea kichwa cha Miguel Gamond na kupima akili yake inawaza nini, kama wengi wetu tunavyojiuliza nani ataanza kwenye kikosi cha kwanza ndiyo swali hilo hilo Miguel Gamond linaishi kwenye ubongo wake muda huu.
.
Ubora wa kikosi umeibua mengi, wengi hawategemea tena mbinu za Miguel Gamondi kufeli kama mitihani ya madenge hata watakapokutana na timu kama Raja Casablanca, ubora umeibua matumaini yaliyoonekana mfu yaonekane yanawezekana kwa macho ya nyama.
.
wananchi sasa wanaiwaza Fainali ya Caf Champion league sio tena makundi, ubora unakuja na gharama. Matokeo yoyote mabovu kinyume na hisia za wananchi yanaweza kuleta gharika isiyoweza kuzuilika.
.
Karata ya kwanza ya Miguel Gamond anaitupa leo dhidi ya Wajerumani, kuifunga Augsburg inaonekana ni kama kujaribu kuigusa mbingu kwa mikono lakini wananchi wameamua kuishi kwenye miujiza hiyo.
.
Malaika wa shari ataanza rasmi kurandaranda kuizunguka akili ya Miguel Gamond leo. Chama, Azizi Ki, Max, Pacome, Mudathir, Abuya nani kuanza? Kama unaona ni rahisi jaribu kukipanga kikosi cha wananchi uone shari itakavyotawala bila kheri.


No comments:

Post a Comment

Pages