HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2024

Matumaini Mapya yawakumbuka wajane Kanisa la Elbethel


Mwenyekiti wa kikundi cha Matumaini Mapya, Theresia Kibona (wa pili kushoto) akikabidhi viti kwa Mchungaji wa Kanisa la Elbethel Raphael Mhagama (wa kwanza kushoto) jijini Dar es Salaam jana wakati wa ibada ya shukrani kwa kikundi hicho.

 

 Na Mwandishi Wetu

KIKUNDI cha Huduma ya Matumaini Mapya, kimetoa msaada wa viti 120 vyenye thamani ya sh. milioni 8.4 pamoja na zawadi kwa wajane na watoto yatima katika kanisa la Elbethel Pentecostal Church for all Nations lilipo Kivule Majohe na Kipunguni jiji ni Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Theresia Kibona akiwa na wanachama wenzake wamekabidhi msaada huo kwenye Ibada maalum ya shukrani kanisani  hapo.

Amesema msaada huo ni  miongoni mwa malengo yao katika kuisaidia jamii  kwa sababu wamejikita  kutoa huduma ya kufundisha neno la Mungu, kuwashauri mabinti na wanawake wanaopitia changamoto  mbalimbali za maisha  kusimama imara ili kutimiza ndoto zao.

“Tunayofuraha kubwa kupata kibali katika kanisa hili, tunamshukuru Mungu wanachama tumetoa fedha kwa ajili ya kununua viti hivi ambavyo vitasaidia  huduma ya Mungu kusonga mbele, ikiwa leo nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa nimefarijika kuwa sehemu ya barakz hizi ambazo naamini zimepata kibali kwa  Mungu,”amesema Theresia.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Suzana Kimambo amesema wametoa msaada wa viti 120 vyenye thamani ya sh. milioni 8.4 pamoja na zawadi nyingine kwa wajane na watoto yatima kanisani hapo.

Katibu wa Kikundi hicho, Loveness Kibona, amesema walianza huduma wakiwa watu 12 na kwamba hadi sasa wamefikia 40, malengo yao ni kuhakikisha wanakuwa sehemu salama ya watu kupata huduma ya neno la Mungu na kupata ushauri nasaha kukabiliana na changamoto za maisha.

Ameongeza wamepanga kuendelea kuisaidia jamii kuwa kuyafikia makundi yote yenye mahitaji kama walivyofanya mwaka 2023 kwa kukitembea kituo cha waraibu wa  dawa za kulevya, kilichopo Pugu ambapo walitoa misaada wa mavazi, chakula na mahitaji mengine.

Akipokea msaada huo Mchungaji wa Kanisa la Elbethel Pentecostal Church, Raphael Mhagama, amewashukuru wanakikundi kwa msaada huo kwa madai walikuwa na uhaba wa viti na tayari walianza kuchangishana ili kuvinunua.

Amesema msaada huo ni muujiza kwao kwani hawakutegemea na kwamba wameweka alama kwa kanisa, kila siku wataendelea kuwaombea ili wabarikiwe kimwili na kiroho kupitia sadaka hiyo walizozitoa kanisani hapo.



No comments:

Post a Comment

Pages