HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 28, 2024

MNEC SALIM SAS KUFANYA ZIARA IRINGA

Na Andrew Chale

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (MNEC) Mkoa wa Iringa Mhe. Salim Abri Asas anatarajiwa kufanya ziara  maalum katika Mkoa huo ambapo pia atakutana na Halmashauri Kuu za CCM Wilaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Iringa imebainisha kuwa ziara hiyo inatarajia kuanzia Mufindi siku ya Jumamosi tarehe 3, Agosti mwaka huu.

" Tarehe 3 Agosti 2024, Mufindi, Tarehe 4, Agosti,  Kilolo.
Tarehe 7 Agosti, Iringa Vijijini na mwisho atahitimisha tarehe 9 Agosti, Iringa mjini.

Mhe MNEC ASAS ameendelea kukiimarisha Chama katika Mkoa wa Iringa huku akiwa nguzo kwenye kushiriki miradi ya kimaendeleo kimkoa, Nyanda za Juu Kusini pamoja na Taifa kwa ujumla.

Pia Mhe MNEC ASAS anasifika kwa Utendajikazi, Upole, Ustamilivu, Subra, Busara, Huruma na Mapenzi yake kwa Chama na Taifa lake vimeendelea kumjengea taswira njema ya Chama kwa Wananchi wote.

Aidha, amekuwa mstari wa mbele kwa kujitolea katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, Mitaji ya Wafanyabiashara wadogo (Machinga), Vijana na Kinamama, Lishe Mashuleni, Michezo na mengine mengi.


No comments:

Post a Comment

Pages