HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 10, 2024

Mwanafunzi KCMUCo ajinyakulia zawadi ya gari Benki ni SimBanking ya CRDB

NA MWANDISHI WETYU, DAR ES SALAAM

 

MWANAFUNZI wa Chuo cha Kikuu Kishiriki cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo) kilichopo Moshi, Hussein Hamisi Hamadi, ameibuka mshindi wa gari ya pili, kati nne zinazotolewa kwa washindi wa Kampeni ya Benki ni SimBanking inayoendeshwa na Benki ya CRDB.


Benki ni SimBanking kupitia kaulimbiu ya ‘Swahiba – Lako, Langu,’ inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kidijitali, ambako washindi wa kila mwezi na kila baada ya miezi mitatu, huzawadiwa zawadi mbalimbali, zikiwemo ‘Tembo Point’ zenye thamani jumla ya Sh. Mil. 200.

 

Kampeni hiyo inatoa zawadi za magari manne aina ya Nissan Dualis (moja kila baada ya miezi mitatu), bajaj 6, bodaboda 12, kompyuta mpakato ‘laptop’ 20, simu janja na ‘Tembo Point’ ambazo mshindi huweza kuzibadili kuwa pesa taslimu na kupewa kiasi cha pointi alizonazo.

 

Droo ya kusaka mshindi wa gari ya pili (wa mwezi Juni), imefanyika jijini Dar es Salaam leo, ambako Hussein amejinyakulia gari hiyo, huku Meneja Mwandamizi wa Huduma za Kibenki Kidijitali wa CRDB, Mangire Kibanda, akisema washindi zaidi wataendelea kuzawadiwa hadi mwisho wa mwaka huu.

 

“Tuko hapa leo kumtafuta na kumtangaza mshindi wa gari la pili la Kampeni ya ‘Benki ni ni SimBanking’, ambako Hussein ameibuka mshindi wetu na amezawadiwa gari aina ya Nissan Dualis, ambayo imekatiwa bima na imejazwa mafuta ‘full tank.’

 

“Lengo la kampeni ni kuchagiza matumizi yasiyo yasiyo ya pesa taslimu ‘cashless,’ badala yake wateja wetu wafanye malipo ya manunuzi kupitia Programu ya SimBanking kama vile kulipia bili za umeme, maji, tiketi za ndege, ada na michango ya shule na kulipia manunuzi ya bidhaa za mtandaoni.

 

“Pia mteja anaweza kushinda zawadi kwa kununua muda wa maongezi, ambako kuna zawadi mbalimbali zikiwemo gari nne, bajaji 6, pikipiki 12, laptop 20 na ‘smartphone,’ na wale watakaoshinda ‘Tembo Point’ wanaweza kuzibadili kuwa pesa taslimu na kuingiziwa kwenye akaunti zao,” alisema.


Aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazokuja na Benki ni SimBanking kwa kufungua akaunti kupitia ‘applications’ ya CRDB, au kupitia mawakala wao na kuunganishwa moja kwa moja na Huduma ya SimBanking, kisha kuingia katika droo za kampeni hiyo.

 

“Baada ya leo kumpata mshindi wa pili wa gari, mwisho wa mwezi ujao pia tutakuwa na droo ya kupata washindi wa bodaboda mbili na bajaj moja, na kila baada ya miezi mitatu, (yaani mwezi wa 9 na mwezi wa 12 mwaka huu), tutakuwa tunakabidhi gari moja moja,” alisisitiza Kibanda.

 

Aidha, Kaulimbiu ya ‘Swahiba – Lako, Langu,’ inayopamba kampeni hiyo, inamaanisha kuwa shida za mteja ndio kipaumbele cha CRDB, ambayo ina mazingira sahihi ya kupata suluhishi za changamoto zozote za kifedha anazoweza kupata mteja wa benki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages