Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amevitaka vyombo vya habari vinavyoripoti taarifa juu ya suala la uibukaji utekaji watoto kupunguza taharuki kwa jamiii kwani inaleta sintofahamu kwa baadhi ya wazazi.
Agizo hilo amelitoa Julai, 24, 2024 ambapo amesema hivi karibuni Temeke kulitokea tukio la mama kiziwi kupigwa na wananchi pasipokuwa na hatia akisingiziwa kuwa ni mtekaji watoto na alihojiwa na polisi na kugundulika kuwa ni kiziwi na alipohojiwa kumbe alikuwa anauliza tu .
"Kwa kweli mimi nimechukizwa sana na baadhi ya vyombo vya habari namna wanavyoripoti matukio haya kwa kuzua taharuki hivyo nitafuatilia na kufikisha kwa mamlaka inayohusika nao ili wawajibishwe kisheria kwani tukiacha waendelee italeta sintofahamu kwa Jamii" amesema Chalamila
Aidha Wananchi watambue kuna vyombo vya ulinzi na usalama wa raia taarifa nyingine wazipuuze kwani kumeibuka baadhi ya wakina mama walezi wamekuwa wakiwaficha watoto na kupigia baba zao simu ili watumiwe hela za matumizi hivyo wameshabainika na wameonywa na Jeshi la polisi ili tabia hiyo isijirudie
July 25, 2024
Home
Unlabelled
RC CHALAMILA; VYOMBO VYA HABARI PUNGUZENI KURIPOTI HABARU ZINAZOLETA TAHARUKI
RC CHALAMILA; VYOMBO VYA HABARI PUNGUZENI KURIPOTI HABARU ZINAZOLETA TAHARUKI
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment