HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2024

DC Mapunda azindua Jengo la Huduma ya Kusafisha Damu, Ambulance

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amezindua Jengo la Kisasa la Kitengo cha Usafishaji wa  Damu (Dialysis) katika  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke (TRRH)  ambalo litakuwa likitoa huduma na matibabu ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo. 
Jengo hilo limekarabatiwa kwa hisani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho kilichopo ndani ya hospitali hiyo Jijini Dar es Salaam imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi.


Akizungumza baada ya uzinduzi wa jengo hilo kwa niaba ya Waziri wa afya Ummy Mwalimu, Mkuu wa wilaya hiyo amesema uwepo wa kituo hicho utapunguza msongamano wa wagonjwa wanaokwenda hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupata huduma ya kusafisha damu(dialysis)ambapo hospitali hiyo Pekee ndiyo iliyokiwa ikitoa huduma hiyo hapo awali.


"Nadhani sasa ujio wa Jengo hili ambalo Lina vifaa vya kisasa Kanisa litatoa matibabu ya huduma za dialysis siyo tu kwa wakazi wa Temeke pekee bali mpaka wale wanaokwenda kuifuata huduma hiyo hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivyo niwapongeze wadau kwa kutoa michango yao ya Hali na mali hasa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) "amesema.

Uzinduzi wa Jengo la kusafisha damu ndani ya hospitali hiyo ambalo lina vifaa vya kisasa vya kutoa huduma ya usafishaji wa damu pia umeenda sambamba na Uzinduzi wa Gari la kubeba Wagonjwa (Ambulance) pamoja na Basi la kubeba watumishi wa hospitali hiyo katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.


Akizungumza kuhusu magonjwa yasiyoambukiza DC Mapunda  amebainisha kuwa  tafiti na tathmini zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyo ya  kuambukiza kama vile Shinikizo la Damu,Sukari,pamoja Afya ya Akili yamekua yakiongezeka kutokana na ulaji usio faa na kutokufanya Mazoezi hivyo niwakati sasa wananchi washiriki kufanya Mazoezi na kuacha kula vyakula  vyenye Chumvi Nyingi na Sukari Nyingi,Pombe kupita kiasi pamoja na Matumizi ya Tumbaku.

"Serikali imeanza kutekeleza Afua mbalimbali ili kukabiliana na Magonjwa haya ikiwemo kufanya uratibu jumuishi wa wagonjwa kuanzia ngazi za zahanati pamoja na kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia wataalamu wa Afya ili kusaidia kukabiliana na Magonjwa haya ambayo yamekua tishio kubwa kwa sasa"amesema DC Mapunda

Awali akitoa taarifa za Utoaji huduma wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke   Mganga  Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Joseph Kimaro amesema kuwa Hospitali hiyo toka kuanzishwa kwake mwaka 1970 imepata mafanikio Makubwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili kama vile Ufinyu wa eneo la Hospitali hiyo kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya utoaji wa huduma kwa Wananchi.

" Tumepata mafanikio makubwa sana kwa sasa tunalaza wagonjwa miambili hamsini(250)hadi mia tatu(300) kwa siku,huku wagonjwa wa nje (OP) ni zaidi ya elfu mbili, hivyo kituo hiki cha kusafishia Damu tunachozindua leo tumepata msaada kutoka kwa wenzetu wa Mamlaka ya Bandari Nchini ( TPA) ambapo wametoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni miambili kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa Jengo la kuweka Mashine,pamoja na shilingi milioni Kumi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kama vile Viti mwendo(Wheelschair? pamoja na vifaa vya Kusafishia Damu" amesema Dkt Kimaro.

Nakuongeza kuwa "Tunaomba  Wadau wengine wajitokeze kutusaidia ili tuweze kuboresha huduma za Wananchi wetu na kumuunga Mkono  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye kwa miaka mitatu ya uongozi wake amewekeza pakubwa kwenye Sekta ya Afya na wananchi wanapata huduma salama.

Mbali na hayo pia Mganga Mkuu huyo aliiomba serikali kuwapatia eneo ambalo wameliomba au kuwapatie eneo lingine kwa ajili ya kuongeza idadi ya majengo ya hospitali kwani kwa sasa kuna ufinyu wa eneo.

 

No comments:

Post a Comment

Pages