HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 13, 2024

ZIFF, EMERSON'S FOUNDATION KUENDELEZA MASHIRIKIANO YA KUKUZA SANAA ZANZIBAR

Na Andrew Chale, Zanzibar

AFISA Mtendaji Mkuu wa Tamasha la Nchi za Majahazi (ZIFF), Joseph Mwale amesema wataendeleza mashirikiano wa kazi za Sanaa na Mfuko wa Wakfu wa Taasisi ya Emerson Zanzibar (Emerson's Zanzibar Foundation) ikiwemo kuibua na kuviendeleza vipaji vya Vijana Visiwani humo.

Joseph Mwale amesema hayo jioni ya Agosti 1
0, 2024 wakati wa sherehe maalum ya tuzo za filamu katika kusheherekea ushindi wa Mohammed Suleiman "Sule" ambaye filamu yake ya 'Uhuru Wangu' Agosti 4 katika kilele cha tamasha la ZIFF 2024 ilishinda Tuzo ya Filamu ya Emerson's Zanzibar Foundation, ambapo amesema kuwa uwezo wa vijana kwenye sekta ya Sanaa hasa filamu Inahitaji kushikwa mkono hivyo kwa namna Bora ya Mfuko huo unahitaji kuendelea kupongezwa na kujivunia.

Aidha, amewapongeza kwa hatua ya kuja na Tuzo ya Uandishi wa Miswada ya Tamthilia 2025 kwani zitaleta chachu kwa Wasanii wa Zanzibar katika ukuaji wao kwenye upande huo muhimu ambao ni Msingi Kwenye masuala ya Uigizaji.

Aidha, Joseph Mwale amesema Emerson's Zanzibar Foundation imekuwa msaada mkubwa kwa ZIFF kwa kuweza kuhamasisha vijana ambao filamu zao zinapata pia kuonekana kwenye Jukwaa hilo kubwa na la Kimataifa la Filamu.

"Emerson's Zanzibar Foundation mnaenda kutusaidia hasa katika hatua yenu hii ya tuzo za Uandishi wa Miswada ya Tamthilia.

Vijana wanaenda kupata ajira lakini pia itaibua kazi nyingi upande huu. ZIFF milango ipo wazi kuendelea kushirikiana kufikia ndoto ya kila msanii sekta ya filamu Zanzibar." Amesema Joseph Mwale.

Aidha, viongozi wa Emerson's Zanzibar Foundation wametangaza rasmi
tuzo hizo za Uandishi wa Miswada ya Tamthilia
2025 ambapo milango ipo wazi kwa watu wote wa Zanzibar.

"Enzi Mpya kwa Uandishi wa Hadithi za Televisheni Zanzibar. Mradi huu maalum umebuniwa ili kuinua sanaa ya uandishi wa miswada ya Tamthilia Zanzibar.

Tuzo hii ya kipekee inalenga kukuza na kutambua vipaji bora vya ndani ya nchi katika uandishi wa miswada, kwa lengo la kuandaa miswada yenye ubora wa hali ya juu inayofaa kwa uzalishaji wa televisheni.

...Katika miaka ya hivi karibuni, tasnia ya filamu ya Tanzania imeona mabadiliko makubwa kutoka kwenye filamu ndefu na fupi kuelekea kwenye Tamthilia za televisheni, ambapo watayarishaji na
waongozaji wameanza kutambua faida za muundo huu.

Uzalishaji wa Tamthilia wa televisheni si
tu kwamba inatoa nafasi ya ukuaji wa haraka lakini pia unatoa fursa endelevu ya mapato, hivyo
kuifanya sekta hii kuwa eneo la ubunifu na ukuaji katika tasnia." Amesema Dismas Sekibaha wa Emerson's.

Aidha, ameongeza kuwa,  Kwa kutoa
jukwaa kwa waandishi chipukizi na wazoefu, tuzo hii inalenga kukuza kizazi kipya cha vipaji vinavyoweza kuunda hadithi zenye mvuto na zinazohusiana na tamaduni za Visiwa vya Zanzibar.

"Kila mwaka, mswada utakaoshinda hautapata tu kutambuliwa bali pia utapata msaada wa
maendeleo zaidi, lengo kuu likiwa ni kuupeleka kwenye kampunin vituo vya televisheni vya
kulipia nchini Tanzania kwa ajili ya uzalishaji na kuoneshwa.

Tuzo hii imepangwa kimkakati kuvutia wawekezaji na wataalamu wa tasnia kwa kutilia mkazo
miswada inayowakilisha kwa kina utamaduni, historia, na hali ya kijamii ya Zanzibar na Tanzania.

Kipaumbele cha kuzalisha maudhui yenye maana na yanayoweza kuuza kibiashara kunahakikisha
kuwa hadithi zinazoundwa sio tu zinavutia bali pia zina uwezo wa kuwa na athari kubwa." Amesema Dismas Sekibaha ambaye ni Mtendaji Mkuu wa mawasiliano ya Umma.

Aidha, amekaribisha wadau kuunga mkono tuzo hizo wakiwemo AZAM MEDIA na DSTV na wadau wengine ambapo pia tuzo hizo zitakuwa nimza kipindi cha miaka mitatu 2025-2027.

Kwa upande wake Mohammed Suleiman ambaye pia ni Rais wa Wasanii wa filamu Zanzibar, amewashukuru viongozi wa Emerson's Zanzibar Foundation kwa kuzo hiyo kwani anaamini hajakata tamaa licha ya kuwa akishiriki mara kwa mara na hatimae amefanikiwa kupata.

Mwaka huu Emerson's Zanzibar Foundation mwaka huu 2024, imetimiza miaka 10, huku mwaka huu ikitoa msimu wa Tisa, upande wa muziki, na upande filamu.

Taasisi hiyo ilianza rasmi, 2014 ikiwa ni mfuko maalum wa Sanaa na Utamaduni.



No comments:

Post a Comment

Pages