HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 09, 2024

Ujenzi wa Ofisi na Maabara za TAEC Zanzibar wakamilika

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) PROF. JOSEPH MSAMBICHAKA amesema uamuzi wa Serikali kupitia TAEC kujenga ofisi na maabara Zanzibar kutasaidia kusogeza huduma ya upimaji wa mionzi karibu na wananchi.

PROF. MSAMBICHAKA ameyasema hayo baada ya kutembelea ofisi na maabaza za TAEC Zanzibar zilizojengwa eneo maalum lililotengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama eneo la viwanda ambapo ujenzi huo wa ofisi na maabara za TAEC umekamilika kwa asilimia 100.

Aidha PROF. MSAMBICHAKA amesisitiza kuwa zamani ilibidi kubeba sampuli kutoka Zanzibar kupeleka Arusha au Dar es salaam kwa ajili upimaji wa mionzi jambo ambalo liligharimu fedha Pamoja na muda ili kupata majibu ambapo kwa sasa upimaji utafanyika Zanzibar jambo litakalosaidia kukuza Uchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. NAJAT KASSIM MOHAMMED ameishukuru serikali kwa kutoa la ujenzi wa ofisi na maabara za TAEC  jambo ambalo litasaidia kuhakikisha  matumizi salama ya mionzi nchini.

 Eneo la viwanda La Dunga Zuze ni eneo maalum lililotengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo lina ukubwa wa hekari 173 na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ndiyo taasisi ya kwanza kujenga ofisi na maabara katika eneo hilo.


No comments:

Post a Comment

Pages