Mwandishi
Wetu, Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi amesema uwepo wa
Muungano umepanua wigo na fursa kwa wananchi katika nyanja za uongozi, biashara
na ajira.
Mhe. Balozi Iddi ameyasema hayo wakati wa
mazungumzo baina yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Massauni alipomtembelea nyumbani kwake
Zanzibar, Disemba 11, 2025 akielezea uzoefu, historia na fursa mbalimbali zilizopo
kupitia Muungano.
Amesema utekelezaji wa masuala
mbalimbali ya Muungano yanayoendelea kufanyika yametokana na utaratibu
uliowekwa, na kuhimiza kila mwananchi kuwa msimamizi na kuwaasa baadhi ya watu
wachache wasiolitakia mema Muungano.
“Kupitia vikao vya pamoja kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar (SMZ), hilo limekuwa ni alama ya kila mmoja kuona namna bora ya
kusimamia maslahi ya Muungano na sio upande mmoja.” Amesema Mhe. Balozi Iddi.
Kwa mujibu wa Balozi Iddi, ameeleza kuwa
Muungano umechukuwa nafasi kubwa katika kuwaunganisha wananchi na kuimarisha
mahusiano mazuri baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na hivyo kuwawezesha
wananchi mpana kwa wananchi kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na
kijamii ili kujipatia maendeleo.
Aidha amesema kuwa Muungano umekuwepo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mahusiano ya karibu na ya kihistoria katika nyanja mbalimbali kama vile udugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa baina ya vyama vya TANU na ASP.







No comments:
Post a Comment