HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 12, 2025

MBUNGE JIMBO LA KILOLO RITHA KABATI AMLILIA JENISTA MHAGAMA

NA DENIS MLOWE, IRINGA


MBUNGE wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Ritha Kabati amewapa pole Watanzania kwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenister Mhagama kilichotokea jijini Dodoma Disemba 11.


Kabati amesema kuwa kifo cha ghafla cha Mhagama amekipokea kwa mstuko mkubwa kwani licha ya kuwa kiongozi katika sekta mbalimbali kama waziri amekuwa chachu kubwa ya wanawake wengi kuingia majimboni kugombea ubunge.

Kabati amesema kuwa licha ya ukubwa aliokuwa nao ndani na nje ya bunge Tanzania imepoteza kiongozi shupavu aliyehuduma katika nafasi zake alizopangiwa kwa weledi mkubwa na viongozi wengi walimwita majina mbalimbali ikiweko kiraka kwani alikuwa kila anapopangiwa alifanya vyema.

Amesema wakazi wa Perahamiho na Tanzania kwa ujumla wamempoteza kiongozi mahiri ambaye atakumbukwa mambo mengi aliyofanya katika nchi na mbaya amefariki ghafla wala hakuwa na taarifa kama ameumwa.

Ameongeza kuwa wakati akiwa waziri wa afya alimwaahidi kuja mkoani hapa kwa aili ya kumpatia tuzo MCC Salim Abri kutokana na kujitoa kwenye jamii ya Iringa endapo angeteuliwa tena katika nafasi hiyo ila imeshindwa kutimia hadi mauti imemkuta.

Aidha amesema kuwa tumuombee na kuenzi mazuri yote aliyofanya enzi za uhai wake kwani anamfahamu Mheshimiwa Mhagama kutokana na uhodari na uwezo wake wa kusimamia ajenda muhimu za wana Peramiho na za kitaifa katika kipindi chote cha utumishi wake akiwa Mbunge na waziri.
 
“Pamoja na salamu hizo za pole kwa familia nampa Pole rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan na ninaungana naye kuendelea kuwasisitiza kumuombea  na kuenzi yote mazuri aliyofanya ili iwe alama ya kumuenzi na kumuombea wakati wote.” Alisema Kabati.


Kabati aliongeza kuwa kutokana na juhudi zake, nilikiri kwamba huyu ndiye mwakilishi wa wananchi. Alikuwa ni shujaa, jambo hilo ni zito, halihimiliki lakini tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atutie nguvu familia yake na watanzania kwa ujumla.





No comments:

Post a Comment

Pages