HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2025

WASTAAFU DODOMA MJINI WANAOLIPWA NA HAZINA WAENDELEA KUPATIWA VITAMBULISHO VYA KIELEKTRONIKI.

Matukio mbalimbali ya zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, kwa muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi tarehe 30 Desemba 2025. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)


 Na Saidina Msangi, WF, Dodoma


Wizara ya Fedha, inaendelea na zoezi la kugawa vitambulisho kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina, katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, kwa muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi tarehe 30 Desemba 2025.



Wastaafu wanaolipwa na Hazina, Wilaya ya Dodoma Mjini, wameendelea kujitokeza kufika katika Ofisi za Wizara ya Fedha ambapo wamepata huduma kwa wakati kutoka kwa watumishi wa Wizara waliojipanga kuhakikisha zoezi hilo linakamilika bila usumbufu.


Wizara ya Fedha inawakaribisha wastaafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini wanaolipwa na Hazina kufika katika Ofisi za Hazina Dodoma, ili kupatiwa vitambulisho vya wastaafu vya kielektroniki kwa muda uliotajwa.

No comments:

Post a Comment

Pages