HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 30, 2026

CRDB Bank Foundation, Enabel zawajengea Vijana Uwezo wa Biashara

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

CRDB Bank Foundation imeendelea kuimarisha juhudi za kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mafunzo ya usimamizi wa miradi, matumizi ya mifumo ya kidijitali na namna ya kupata mitaji ili kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi.


Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Kilimo Biashara wa CRDB Bank Foundation, Maregesi Shaaban, amesema lengo ni kuwajengea washiriki uwezo wa kusimamia vyema miradi ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwafahamisha fursa za kupata mitaji kupitia kampuni tanzu ya CRDB Bank Foundation.



Amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza maarifa ya washiriki ili waendane na mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea duniani, huku wakitumia mifumo ya kidijitali kuboresha biashara zao na kupata huduma za kifedha kwa urahisi.


“Leo mteja wa CRDB anaweza kufungua akaunti, kufanya miamala, kupata taarifa za akaunti na hata kuomba mkopo kupitia simu ya mkononi bila kufika tawi. Hii ndiyo dunia tunayoielekea, hivyo ni muhimu kuwajengea uwezo wananchi kutumia teknolojia kwa maendeleo yao,” alisema.



Shaban aliongeza kuwa ushirikiano kati ya CRDB Bank Foundation, Enabel na Umoja wa Ulaya unalenga kuandaa rasilimali watu wenye ujuzi utakaosaidia kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yenye lengo la kujenga uchumi wa zaidi ya dola trilioni moja.


Kwa upande wake, Meneja Mradi Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (Enabel), Kikolo Mwakasungula, amesema mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya unatekelezwa katika mikoa ya Mwanza, Tanga na Pemba, ukilenga kuwawezesha vijana kupitia mafunzo ya biashara, upatikanaji wa mitaji na kukuza uchumi wa kijani pamoja na uchumi wa mzunguko ili kuboresha maisha yao.



No comments:

Post a Comment

Pages