HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 31, 2026

CRDB Yawahimiza Vij CRDB Yawahimiza Vijana Kujiongezea Ujuzi kwa Ajira na Biasharaana Kujiongezea Ujuzi kwa Ajira na Biashara

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


Benki ya CRDB imewahimiza vijana nchini kutambua kuwa mafanikio yao yanategemea juhudi binafsi za kujiendeleza, huku ikisisitiza umuhimu wa kuongeza ujuzi unaokwenda sambamba na mahitaji ya soko la ajira na biashara.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwawezesha vijana yaliyoandaliwa na Jigundue Organization na kuwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Geoffrey Rutasingwa, alisema elimu ya darasani ni msingi muhimu lakini haitoshi bila juhudi za mtu binafsi kujifunza ujuzi mpya.



Alisema vijana wa sasa wana fursa kubwa zaidi kutokana na maendeleo ya teknolojia, upatikanaji wa taarifa kwa urahisi na uwezo wa kutumia mifumo ya kidijitali, hivyo wanapaswa kutumia mazingira hayo kujijengea uwezo wa kushindana katika ajira na biashara.


Rutasingwa alisema jukumu la kuziba pengo kati ya elimu ya darasani na mahitaji halisi ya soko la ajira lipo mikononi mwa vijana wenyewe kwa kuendelea kujifunza, kuboresha tabia za kazi na kujiamini katika kutumia vipaji na uwezo wao.



Aliongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili vijana wengi ni kushindwa kutambua uwezo walionao na namna ya kuutumia kuzalisha fursa za maendeleo, licha ya kuwa na rasilimali nyingi za kujifunzia kupitia teknolojia.


Aidha, alisema uwekezaji kwa vijana ni moja ya nguzo za mkakati wa Benki ya CRDB wa miaka mitano (2022–2027), ambapo kupitia programu ya Imbeju benki imeendelea kutoa mitaji nafuu, mafunzo na fursa mbalimbali za biashara kwa vijana na wanawake.



Kwa mujibu wa Rutasingwa, zaidi ya vijana 10,000 tayari wamenufaika na programu hiyo, huku zaidi ya Sh bilioni 10 zikiwa zimetolewa kama mikopo wezeshi kwa vijana na wanawake ili kuwawezesha kujiajiri na kukuza biashara 

No comments:

Post a Comment

Pages