Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimepokea ugeni kutoka Chama cha Waandishi wa Habari cha Oman (Omani Journalists Association - OJA), leo, Agosti 18, 2026.
Taarifa ya ujio wa ugeni huo imetolewa na Katibu Mkuu wa JOWUTA, Selemani Msuya ambaye amesema wameuchukulia kwa uzito ugeni huo kutoka Oman.
"Ugeni huu muhimu ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na JOWUTA katika nyanja mbalimbali, ikiwemo eneo la kitaaluma," alisema Msuya.
Msuya alisema ugeni huo wa wajumbe wanne kutoka Oman utakutana na viongozi wa JOWUTA, ambapo mazungumzo yatajikita katika kuandaa kongamano litakalojulikana kama Oman – Tanzania Journalists Forum.
Alisema viongozi watajadiliana kuhusu ushirikiano baina ya JOWUTA na OJA, Programu za kubadilishana uzoefu baina ya waandishi wa habari wa Tanzania na Oman.
Katibu mkuu huyo alisema ugeni huo unatarajiwa kukutana na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Maliasili na Utalii, kabla ya kwenda Zanzibar baadaye.





No comments:
Post a Comment