Na John MARWA
BILA shaka moja kati ya wimbo ambao mashabiki wa Simba watapenda kuusikiliza na kujihimu katika maombi ni ‘Nikumbuke’ ya Joel Lwaga mkali wa gospel aliyemshirikisha Diamond Platinumz, ikiwa leo oktoba 10 kwenye mchezo wa (NBC PL) dhidi ya watani zao Yanga SC.
Simba na Yanga zitashuka dimbani jioni ya leo katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam, mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi msimu huu, huku kila timu ikiwa na wastani wa asilimia miamoja za ushidi katika michezo ambayo wamecheza.
Ni mchezo ambao Simba watakuwa nyumbani, huku kumbukumbu zikionyesha mara ya mwisho Mnyama kupata ushindi dhidi ya Yanga ni April 16, 2023, wa mabao 2-0, uwanja wa Benjamin Mkapa. Baada ya hapo Lunyasi hawajapa ushindi wowote kwenye Ligi katika misimu miwili iliyofuata.
Yawezekena Simba hawateseki na namna Yanga wanavyowanyanyasa lakini wana wivu wa kupata pointi tatu dhidi yao, hapo si watakuwa sawa, ama watakuwa wanamkumbusha Mungu wao awakumbuke nao furaha yao?
Wana Msimbazi nao ni binadamu, mioyo imizidiwa, na wamechoka, watamweleza nani kama sio muumba wao, kuelekea dakika 90 za leo, maana anawajua na anajua wanachopitia, watamuomba nani kama sio yeye, awakumbuke kwenye riziki ya kicheko chao?
Je itakuwa rahisi maombi yao kusikika ama Wananchi nao watajipenyeza na kuomba maombi yao, ya kuwa riziki ni mafungu saba, pengine zamu bado ni ya kwao waendeleee kufurahika?
Hata kama wao sio wema sana, lakini, hawataomba ikimpendeza aliye juu, basi vicheko viendelee hata kama ni msimu wa 10 mtawalia, kwa furaha wafarijike hata hii leo?
Ni sala na maombi ya nani kusikika na kukumbukwa kwenye Derby ya Kariakoo ndani ya mitaa ya Temeke, huku kila timu ikionyesha kuwa na utayali wa kusaka heshima na kuendeleza heshima msimu huu.
Ni vita ya mbinu, ufundi na utayali huku sala, maombi na dua zikiisindikiza miongoni mwa Derby kubwa Barani Afrika kutoka kwenye Ligi Bora kusini mwa Jangwa la Sahara.
October 10, 2026
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.





No comments:
Post a Comment