HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

November 16, 2026

CRDB YAENDELEA KUWA NA WASTAAFU

WASTAAFU wametakiwa kutumia uzoefu, maarifa na muda walionao baada ya kumaliza utumishi rasmi kujiingiza katika shughuli za uzalishaji mali na kuchangia maendeleo ya jamii, badala ya kuona kustaafu kuwa mwisho wa shughuli zao za kiuchumi.


Wito huo umetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima, aliyesema kipindi cha kustaafu kinaweza kuwa fursa ya kutimiza malengo mbalimbali ambayo watu walishindwa kuyafikia walipokuwa katika ajira.


 

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Kongamano la Wazee lililoandaliwa na Benki ya CRDB, Dk. Gwajima amewahimiza wastaafu kujikita katika shughuli mbalimbali zikiwemo biashara, kilimo cha kisasa, ufugaji na uwekezaji wa nyumba za kupangisha.

Amesema uzoefu walioupata katika kipindi chote cha utumishi unaweza kutumika kuanzisha shughuli za kiuchumi, kubuni fursa mpya na kutoa mchango wa kitaalamu kwa jamii.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwaandaa watumishi wanaokaribia kustaafu kwa kuwapatia elimu itakayowawezesha kukabiliana na maisha baada ya ajira, hususan katika masuala ya uwekezaji, matumizi ya teknolojia na ushiriki katika shughuli za maendeleo.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa, amesema benki hiyo itaendelea kuwa karibu na wateja wake hata wanapomaliza utumishi kupitia mpango wa Swahiba Mstaafu.


 

Amesema mpango huo unalenga kuwasaidia wastaafu kukabiliana na mahitaji yao ya kifedha na kijamii, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuwapatia huduma katika hatua mbalimbali za maisha yao.

No comments:

Post a Comment

Pages