HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 09, 2013

KAMPUNI YA PUMA YAINGIA MKATABA KUIVALISHA ARSENAL


Juu: Logo ya 'Washika Bunduki' Arsenal FC. Chini: Mashabiki wa soka nje ya Uwanja wa Emirates jijini London, unaomilikiwa na Arsenal


LONDON, England

Mkataba wa sasa wa Arsenal na Kampuni ya Nike, wenye thamani ya pauni milioni 55 kwa miaka saba – unafikia tamati mwishoni mwa msimu ujao


KLABU ya Arsenal, imeingia mkataba wa jezi na vifaa vya michezo na Kampuni ya Puma wenye thamani ya pauni milioni 170, unaohitimisha miaka 20 ya Washika Bunduki hao kuvalishwa na Kampuni ya Nike.

Mtendaji Mkuu wa Gunners, Ivan Gazidis ametiliana saini na Puma ya kuivalisha Arsenal kwa miaka mitano, mkataba unaomaanisha kuwa klabu itapokea vifaa vyenye zaidi ya pauni milioni 30 kwa mwaka.

Mkataba wa sasa wa Arsenal na Kampuni ya Nike, wenye thamani ya pauni milioni 55 kwa miaka saba – unafikia tamati mwishoni mwa msimu ujao.

Arsenal imekuwa ikikataa mikataba ya muda mrefu tangu ilipohamia kwenye dimba la Emirates kutoka lile la zamani la Highbury mwaka 2006.

Lakini sasa imeanga mbele na kujaribu kutanua wigo wa miakataba mipya na yenye tija.

Nike ilikuwa ya kwanza kukataa makubaliano ya mkataba mpya Gunners, na kuamua kutofanya maboresho na nyongeza ya mkataba wa sasa.

Gunners inayonolewa na Arsene Wenger, ilitangaza na kufuata sera za kubana matumizi yake kwa kila msimu, tangu ilipohama Highbury, miaka saba iliyopita.

Sera hiyo inapingwa na mashabiki wa timu hiyo, wanaoumizwa na ukame wa mataji wa miaka minane sasa, na wanaona timu yao inaweza kushindana na klabu zinazotumia pesa kubwa England za Man United, Man City na Chelsea kupitia pesa za udhamini.

The Sun

No comments:

Post a Comment

Pages