Meneja wa Bia ya Safari, Oscar Shelukindo akifafanua jambo kuhusu fainali za Pool
Lwiza Mbutu akizungumza na waandishi wa habari.
Mchezaji wa Single wa Chuo cha CBE, Liliani Meori
Katibu wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Amos Kafwinga akizungumza wakati wa mkutano huo.
Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Mbutu akionesha manjonjo yake wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. Kushoto ni Rapa wa bendi hiyo, Jumainn Said.
Na Mwandishi Wetu
BENDI
ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta, inatarajia kupamba fainali za Michuano ya
mchezo wa Pool ngazi ya Taifa yajulikanayo kama
'Safari Lager Higher Learning Competition 2013'.
Fainali
hizo zinatarajiwa kupigwa katika viwanja vya Leders kuanzia kesho mpaka
Jumapili ambapo anatarajiwa kupatikana bingwa wa michuano hiyo iliyoanza
kutimua vumbi Mei 5 mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Safari Lager
ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Oscar Shelukindo alisema, wameamua
kuichukua bendi ya Twanga ili kutoa burudani wakati wa fainali hiyo ambayo pia
itapabwa na nyama choma kutoka katika bar tano zilizoshinda katika shindano la
nyama choma mwaka huu.
Shelukindo
alisema, bingwa katika shindano hilo
atajinyakulia kitita cha sh mil 2.5 pamoja na kombe huku zawadi nyingine
zikitolewa kwa mshindi wa pili na mchezaji mmoja mmoja na kudai kuwa, timu nane
zitachuano ambao ni mabingwa wa kila Mkoa.
Nae
Kiongozi wa bendi ya Twanga Luiza Mbutu alisema, wamejipanga kufanya burudani
kali ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha wapenzi na mashabiki wao nyimbo mpya na
kuwataka kuja kwa wingi kwani hakuna kiingilio.
Katika
fainali hizo bingwa mtetezi ni chuo cha Sauti Mwanza ambacho pia kimefanikiwa
kuingia katika kinyanyang’anyiro hicho mwaka huu.
No comments:
Post a Comment