Spika wa Bunge amesema Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unafanyika wakati Tanzania ikiwa imefanya juhudi kubwa kujenga utawala bora, Imani ya jamii na fursa jumuishi za kijamii na kiuchumi.
Mheshimiwa Spika amesema katika kipindi hiki, Tanzania imeshuhudia mageuzi ya kisiasa na maridhiano ambapo Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliendeleza falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Kujenga Upya).
Amesema falsafa hiyo imetoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya haki za binadamu, demokrasia na utawala jumuishi.
“Kufuatia mageuzi haya, Bunge la Tanzania lilipitisha sheria kadhaa za mageuzi ya kisiasa, ikiwemo Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Serikali za Mitaa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa.
“Sheria hizi zinalenga kuhakikisha michakato ya uchaguzi iliyo huru, yenye uwazi na inayoaminika zaidi,” amesema.
October 07, 2026
Home
Unlabelled
Spika: Tanzania imeimarisha utawala bora na fursa jumuishi kwa jamii
Spika: Tanzania imeimarisha utawala bora na fursa jumuishi kwa jamii
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.





No comments:
Post a Comment