Na Elizabeth John
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Dully Sykes amewashauri wasanii wenzake kuitafuta zaidi elimu ya darasani ili iweze kuwasaidia katika suala zima la wizi wa kazi zao.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Dully alisema wasanii wengi wa bongo fleva wanabebwa na vipaji walivyo navyo, si elimu.
“Kunawasanii hapa Tanzania wanaibiwa kazi zao kila siku kwa sababu hawajasoma na hawaelewi mikataba na mambo mengi tu, wanabaki kudhulumiwa na mameneja wao,” alisema Dully.
Alisema jasho la wasanii huibiwa kila siku hususani mauzo ya albamu na miito ya simu sababu ni kukosa elimu.
Nyota huyo ambaye anamiliki studio mbili za kurekodi muziki, Dhahabu record na 4.12 record alisema wasanii wa bongo wanatakiwa wasome ili muziki wetu ufike mbali na sio kuishia hapa.
Alisema kutokana na kuufahamu umuhimu wa elimu anatamani apate mwalimu wa kumfundisha nyumbani kutokana na kukosa nafasi ya kwenda darasani.
No comments:
Post a Comment