HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 30, 2013

Q CHILLAH AMUANIKA BEAUTIFUL



Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Abubakar Shaaban 'Q-Chilla' anatarajia kuachia kazi yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la 'Beautiful'.

Alisema jana kuwa, maandalizi ya kazi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho muda wowote inakapokuwa tayari ataisambaza katika vituo mbalimbali vya radio.

"Naamini kazi hiyo itapokelewa vizuri na mashabiki kutokana na upangiliaji wa mashairi yenye ujumbe kwa jamii na yenye lengo la kuburudisha, kuelimisha na kukosoa jamii," alisema.

Alisema hawezi kuweka wazi ni lini ataisambaza kazi hiyo ila anawataka mashabiki kukaa mkao wa kupokea kazi hiyo ambayo ipo katika hatua zamwisho za kukamilika.

Nyota huyo mbali na kutaka kuachia kazi hiyo alishawai kutamba na kazi kama  Ninachokipata,  Chameleon, Nonino, na Domokaya.

No comments:

Post a Comment

Pages