Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya
uhamiaji wakati alipowasili kwenye jengo la Idara hiyo mjini Songea kuweka jiwe
la msingi akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mabwawa ya kufugia samaki wakati alipotembelea
Kituo cha Maendeleo ya Ufugaji Samaki cha Ruhila kilichopo mjini Songea.
Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama chakula cha samaki wakati alipotembelea Kituo cha
Maendeleo ya Ufugaji wa Samaki cha Ruhila kilichopo Songea Mjini akiwa
katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 20, 2013. Wapili kulia ni mkewe, Mama Tunu
Pinda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto kwake) wakitazama ngoma ya
wanawake wa Songea kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafnzi wa Shule ya Sekondari ya Songea
Girls baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Songea Julai 20, 2013.
Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
Baadhi ya Waislam walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda kwenye Ikulu ndogo ya Songea wakishiriki katika futari hiyo.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda
(wapili kulia) akizungumza na baadhi ya wanawake walioshiriki
katika futari ambayo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaandalia baadhi ya Waislam wa
Songea.
No comments:
Post a Comment