Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Bima ya CRDB imezindua kampeni maalumu ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa bima, ikihamasisha jamii kutambua kuwa kinga ni bora kuliko tiba kwa kulinda maisha na mali zao mapema.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya CRDB, Wilson Mzava, alisema kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu usalama, uwajibikaji na umuhimu wa kujiandaa mapema kwa kulinda mali na maisha kupitia huduma za bima.
Mzava alisema mbali na kutoa elimu, kampeni hiyo pia inalenga kujenga uhusiano wa karibu kati ya wananchi na huduma za bima kwa kuzungumzia changamoto na hali halisi wanazokutana nazo katika maisha yao ya kila siku.
Aidha, Kampuni ya Bima ya CRDB imemtambulisha mfanyabiashara na msanii Hamisa Mobetto kuwa balozi wa kampeni hiyo, ambapo atashiriki kufikisha elimu ya bima kwa umma na kuhamasisha wananchi kutumia huduma hizo kwa ajili ya kujikinga na majanga mbalimbali.




No comments:
Post a Comment