Mshindi
wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Fabian Nelson (Tanzania) katika
Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) Nchini Nambia akishangilia na bendera ya taifa mara baada
ya kumaliza mbio hizo katika uwanja wa taifa wa Namibia (Picha zote na Frank
Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Mshindi
wa kwanza katika mbio za mita 10000 kwa Wanaume Fabian Nelson (Tanzania)
akivalishwa medali ya dhahabu na mmoja wa makamishna wa Polisi wa Namibia
katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) katika uwanja wa taifa wa Namibia.
Baadhi
ya wanamichezo wa Tanzania wakishangilia ushindi wa kwanza katika mbio za mita
10000 kwa Wanaume katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini
mwa Afrika (SARPPCO) katika uwanja wa
taifa wa Namibia.
Wanaridaha wa mbio za mita 10000 kwa Wanaume wakikimbia
katika Michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kwa Nchi za kusini mwa Afrika (SARPPCO) Nchini Nambia.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek
Wanariadha wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa wakuu wa
Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO nchini Namibia wameanza vyema mbio hizo
baada ya kufanikiwa kunyakua medali za Dhahabu na fedha katika mbio za mita
elfu 10000 wanaume.
Aliyenyakua medali ya dhahabu ni Mwanariadha Fabian Nelson
ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania ) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde
45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe ,Namibia ,Botwasana
na Angola .
Wengine walioipatia Tanzania Medali ni pamoja na Basili
John mita 800 (Shaba ) na Mohamed Ibrahim mchezo wa kurusha
kisahani (shaba ).
Katika mpira wa miguu mechi ya ufunguzi ilizikutanisha
wenyeji Namibia na Msumbiji
ambapo Namibia iliichapa
Msumbiji mabao 2 kwa 0 huku kwenye mpira wa miguu wanawake Namibia na Angola zilitoka suluhu ya bila
kufungana.
No comments:
Post a Comment