Jaji Mkuu wa shindano la kuimba
la Epiq BSS, Ritha Paulsen, akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo
ya shindano hilo. Anayemfuatia ni meneja wa vipindi wa TBC, Edna Rajab na
Walter Chillambo, mshindi wa shindano hilo mwaka jana.
Mshiriki
wa shindino la kuimba la Epiq BSS, Menina Atick ambaye aliingia kwa njia ya
usaili wa simu, akimkabidhi jaji mkuu wa shindano hilo Ritha Paulsen video ya
wimbo wake.
·
Inaonyeshwa
TBC Taifa Jumapili saa tatu usiku na kurudiwa jumatano saa 8
·
Imepata
mafanikio makubwa mikoani
·
Usaili
kwa njia ya simu unaendelea
Dar es Salaam, 21-8-2013: Shindano la kuimba la Epiq BSS
limetangaza kuwaingiza washiriki wake waliongia 20 bora kambini, ili waanze
mafunzo mapema na kutoa washiriki bora zaidi mwaka huu.
Shindano hilo ambalo kwa mwaka huu linarushiwa kwenye kituo cha
televisheni cha TBC, kila Jumapili saa tatu usiku na kurudiwa kila jumatano saa
nane mchana, limevuta mashabiki wengi nchini kwa burudani wanayoipata.
‘Mwaka huu washiriki waliongia ishirini bora wataingia kambini
mapema zaidi, ili kuhakikisha wanajifunza mambo mengi, hali itakayoleta
ushindani zaidi pamoja na kuzalisha washiriki ambao watafanya vizuri kwenye
soko’ alisema Ritha.
Ritha pia amefurahishwa na mafanikio makubwa ambayo Epiq BSS
limepata mikoani, kwa idadi nzuri ya vijana waliojitokeza lakini pia ubora wa
vipaji vilivyojitokeza.
“Tumepata washiriki mahiri kutoka mikoa mbalimbali,hivyo
mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkali sana na ninaamini tutapata
wasanii bora zaidi kuliko miaka iliyopita” alisisitiza Ritha.
Kwa upande wake Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan,
alisema kampuni yake imedhamiria kuboresha shindano hilo mwaka huu kwa kuongeza
vitu mbalimbali.
‘Kwa hakika tumefanikiwa kuboresha shindano kwa kiasi kikubwa,
lakini pia tumehakikisha washiriki waliopita wanaendelea vizuri, mfano mzuri ni
Walter na Menina ambao wanafanya vizuri kwenye soko’ alisema Khan.
Usaili
wa Epiq Bongo Star Search kwa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita ya Arusha,
Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na kumalizia Dar es Salaam.
Washiriki
50 walipatikana kutoka mikoa yote, na wamechujwa na kubakia washiriki 20 ambao
ndio watakao ingia kambini.
Washiriki
wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba 0901551000
au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna ya kujiunga.
No comments:
Post a Comment