Na Walter Mguluchuma, Mpanda Katavi
Fundi baiskeli mmoja Mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Athumani Mussa (54) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumlawiti (kunajisi) mdomoni mtoto wa miaka 4 baada ya kumdanganya kumpatia mdoli wa kuchezea
Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka mkaguzi wa msaidizi wa polisi Razalo Masembo mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa.
Mwendesha mashika aliimbia mahakama kuwa mshitakiwa Athumani Mussa alitenda kosa hilo hapo julai 24 mwaka huu majira ya saa 12 jioni nyumbani kwake katika Mtaa wa Nsemlwa mjini hapa.
Mtuhumiwa anadaiwa siku hiyo ya tukio alimwona mtoto huyo akiwa na wenzake wakicheza barabarani karibu na nyumbani kwake ndipo alipo mwita mtoto huyo na kumwambia amfuate nyumbani kwake ili akampe mdoli wa kuchezea.
Mwendesha mashitaka aliendelea kueleza kuwa mara baada ya mtoto huyo kuingia ndani mtuhumiwa alianza kumlawiti ( kumnajisi) mtoto huyo mdomoni huku akiwa amekaa kwenye kochi lake sebuleni.
Ilidaiwa licha ya mtoto huyo kupiga mayowe ya kuomba msada mtuhumiwa hakujali mayowe ya mtoto huyo bali aliendelea na shughuli yake hadi hapo alipo maliza haja yake hiyo ya kumlawiti mdomoni.
Mwendesha mashitaka alidai kuwa mtoto huyo alipo toka nyumbani kwa mtuhumiwa alielekea nyumbani kwa mama yake huku akiwa akilia kwa sauti kubwa hari iliyo pelekea watoto wenzake wamfuate kwa nyuma
.
Masembo alieleza mara baada ya kufika kwa mama yake na alipoulizwa analia nini mtoto huyo alitema mdomoni mbele ya mama yake mbegu za kiume na kisha alimweleza mama yake kuwa amelawitiwa mdomoni na fundi baiskeli anaitwa Mussa
Mama wa mtoto huyo baada ya kujua mwanae amelawitiwa mdomoni alianza kuangua kilio na kufanya majirani wkusaniyike hapo ndipo alipo waeleza mkasa huo aliofanyiwa mwanae na mtuhumiwa.
Majirani hao ndio walipo chukua jukumu la kwenda kumkamata mtuhumiwa wakiwa wanaongozwa na mtoto huyo ambae awali alikuwa amekataa kuingia ndani ya nyumba hiyo ya mtuhumiwa kwa kile alidai anaogopa kulawitiwa tena na mtuhumiwa
Mtuhumiwa Athumani Mussa alikana shitaka hilo na Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa aliamuru mshitakiwa apelekwe rumande hadi hapo septemba 2 kesi yake itakapo sikilizwa
No comments:
Post a Comment