HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 17, 2014

Mwanafunzi wa kidato chatano ajinyonga akiwa hospitalini huku akiacha ujumbe mzito

Na Ashura Jumapili, Bukoba,

MWANAFUNZI  wa  kidato cha tano Ezra Gerald  Wambamba (19 )wa kombi ya CBG katika shule  ya sekondari  ya wavulana  Ihungo  iliyoko  Manispaa ya Bukoba Mkoani  Kagera,  amejinyonga kwa kutumia shuka hadi kufa kwa madai ya kukosa huduma ya matibabu akiwa hospitali.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Kagera,  Gilles  Muroto, amesema kuwa  tukio  hilo lilitokea  Septemba 16 mwaka huu  majira  ya saa moja, asubuhi  katika  hospitali ya  Mkoa  wa Kagera, alikokuwa amelazwa mwanafunzi huyo anayetoka maeneo ya Kitete mkoani Tabora.

Muroto,alisema, mwanafunzi huyo alijinyonga kwaku tumia  shuka hadi kufa umbali wa mita 73 kutoka wodi namba tatu alikokuwa,amelazwa mwanafunzi huyo alifunga  shuka hiyo juu ya mti na kujinyonga.

Alisema,alilazwa hospitali hapo tangu  Septemba 11 mwaka huu na kugundulika kuwa anasumbuliwa na homa ya typhoid  hadi 16 alipoamua kujinyonga.
Alisema,mwili wa marehemu, ulipopekuliwa na  jeshi la polisi alikutwa na kipandae cha karatasi kilichoandikwa ujumbe unaosemeka hivi ”haiwezekani  binadamu kuhudumiwa kama mbwa yaani nafika hospitali najieleza  hali yangu halafu daktari ananiandikia  kulazwa  bila kupimwa,sasa sijui natibiwa nini?kwakweli siwezi kuvumilia yaani wenzangu wanasoma halafu mimi nimekalishwa  tu hapa hosipital  bila ya kujua natibiwa  nini?,inaniuma  sana mpaka kufikia hatua hii kujiondoa  duniani kwa sababu ninaona watu
wanachezea   ndoto zangu mimi siwezi kuona ndoto  yangu inazimwa wakati inatakiwa  niwepo shuleni nikamilishe ndoto  zangu.”

Alisemabaada yakuandikaujumbehuoakamaliziakwakusema “mjitahidi tukutane mbinguni”mwishoakaandikanenolakiingereza( respect myfamily and Henry).


Aliongeza kuwa katika tukio  hilo hakuna ,aliyekamatwa  uchunguzi unaendelea kuhusiana na kifo hicho cha mwanafunzi.

Kwa upande wake katibu wa hospitali ya mkoa wa Kagera  Benges Justus alithibitisha kutokea kwa tukio la mwanafunzi  kujinyonga hadi kufa septemba 16 mwaka huu majira ya saa moja na nusu asubuhi.

Benges,alisema mwanafunzi huyo alipokelewa  hospitalini hapo septemba 15na baada yakufanyiwa uchunguzi wa kitabibu wa vipimo vyote ilibainika kuwa anasumbuliwa na maralia hivyo kuanzishiwa tibaya  maralia.

Alipohojiwa  kamamgonjwa huyo alikuwa na typhoid alisema vipimo vilionyesha maralia na siyo typhoid.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyo unaendelea ilikubaini kilichomuua. Chanzo cha habari Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment

Pages