Washiriki wa Fainali za Mashindano ya urembo ya Redds Miss
Tanzania 2014 kutoka mikoa mbalimbali nchini wataanza kambi rasmi ya mafunzo
kwa kuingia kambini Jumamosi ya tarehe 13 Septemba 2014.
Washiriki hao 30 watapiga
kambi katika Hotel ya JB Belmont iliyopo
katikati ya jiji ya D’salaam ambapo mazoezi na mafunzo ya aina mbalimbali
yatatolewa kwa muda wa wiki nne kabla ya Fainali za Taifa ambazo zimepangwa kufanyika
mapema mwezi ujao.
Wakiwa kambini warembo hao watapewa semina kuhusu masuala
mbalimbali yanayohusu mashindano ya
urembo, kusaini Mikataba n.k.
Kwa mujibu wa Ratiba ya Kambi iliyotolewa na Lino International
Agency Limited, waandaji wa Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, washiriki
hao watakuwa hotelini hapo kwa muda wa siku 3 tu, na baadaye kuanza ziara ya
kutembelea Vivutio mbalimbali vya Utalii
katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha.
Washiriki hao watarejea jijini D’salaam tarehe 28 Septemba 2014
na kufikia katika hotel ya Kijiji Beach
Kigamboni na kuendelea na ratiba yao
ya mafunzo kama ilivyopangwa na
waandaji.
Orodha ya washiriki pamoja na mikoa wanayowakilisha
imeambatanishwa.
Shindano la Redds Miss Tanzania linadhaminiwa na REDDS ORIGINAL.
No comments:
Post a Comment