HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 01, 2014

TRENI YA AIRPORT KUANZA DECEMBA

KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka, amesema serikali inatarajia kuanzisha usafiri wa treni kutoka katikati ya jiji hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JKNIA), ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa

Dk Mwinjaka aliitoa kauli hiyo  jijini Dar es Salaam wakati alipokua akinadi vivutio mbalimbali vya uwekezaji kwa Wawekezaji kutoka nchini Marekani, ambapo wamo wanaohusiana na sekta ya usafiri wa reli.

Alisema kuanzishwa kwa usafiri huo kutasaidia kupunguza hali ya usafiri tata wa kutoka katikati ya jiji hadi uwamja wa ndege na Gongolamboto, ambapo majadiliano ya kuanzisha usafiri huo, yako katika hatua za mwisho kati ya wanasheria wa wizara na wale muwekezaji kutoka Marekani.

“Wakezaji hawa wapatao 12 waliokuja ni matunda ya ziara ya Rai Jakaya Kikwete aliyoifanya hivi karibuni, ambapo wako katika maeneo mbalimbali ya Bandari, Reli na yule atakayesaidia kuanzisha usafiri wa treni kuelekea Gongolamboto ambaye ametuonyesha aina ya treni inayoweza kutumika katika reli yetu,”alisema Dk Mwinjaka.

Hata hivyo, alisema baadhi ya wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo ya bandari nchini ambapo watapelekwa katika bandari ya Dar es Salaam lakini kipaumbele ni kwa sasa ni Mtwara.

Dk Mwinjaka, alisema Mtwara imepewa nafasi kubwa katika uimarishaji wa bandari yake, hiyo inatokana ugunduzi wa gesi na miradi mingine ya makaa yam awe na chuma chapua ambapo vyote hivyo vitahiji kusafirishwa kwa haraka kupitia bandari hiyo.

“Wapo walionesha nia ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Reli ya Kati sasa hawa tutawaelekeza katika Idara zinazohusika kama vile Rahako,”alisema Dk Mwinjaka.

Akizungumzia kuhusu ajali zinazotokea, alisema baadhi ya wawekezaji hao wako tayari kuwekeza katika kuingiza vifaa vya kisasa ambavyo vitaweza kuayagua magari ambayo hayata kuwa na vigezo vitakavyoruhusu yatembee barabarani kama ilivyo sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages