KAIMU Ofisa wa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Pwani, Dismas Chuwalo, ameishauri serikali kufuta ada
ya shule za sekondari za Kata ili wahitimu wote wanaochaguliwa waweze kujiunga
na shule hizo.
Chuwalo, alitoa
kauli hiyo wakati wa mahafali ya pili ya shule ya msingi Calvary Montesori,
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema wazazi
wengi waliopo maeneo ya vijijini wanashindwa kuwapeleka watoto wao kujiunga na
kidato cha kwanza katika shule hizo kutokana na kushindwa kulipa ada na
michango mingine mbalimbali.
Aliwataka wazazi
kuhakikisha wanatenga muda wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao, ikiwa ni
pamoja na kukagua madaftari.
Mkurugenzi wa
Shule hiyo, Sibonike Mponzi, alisema ya shule hiyo imekuwa na mafanikio ya
kitaaluma kutokana na uongozi kutoa motisha kwa walimu kila mwaka tangu
ilipoanzishwa.
Alisema ili
shule za serikali zifanye vizuri katika ufaulu, ni vema ikawapatia walimu
motisha na kuwajengea mazingira bora ya kazi katika shule wanazofundisha.
No comments:
Post a Comment