KATIBU Mkuu
Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka, amesema serikali inatarajia kuanzisha
usafiri wa treni kutoka katikati ya jiji hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Kambarage Nyerere (JKNIA), ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa
Dk Mwinjaka
aliitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipokua akinadi vivutio mbalimbali vya uwekezaji kwa Wawekezaji
kutoka nchini Marekani, ambapo wamo wanaohusiana na sekta ya usafiri wa reli.
Alisema
kuanzishwa kwa usafiri huo kutasaidia kupunguza hali ya usafiri tata wa kutoka
katikati ya jiji hadi uwamja wa ndege na Gongolamboto, ambapo majadiliano ya
kuanzisha usafiri huo, yako katika hatua za mwisho kati ya wanasheria wa wizara
na wale muwekezaji kutoka Marekani.
“Wakezaji
hawa wapatao 12 waliokuja ni matunda ya ziara ya Rai Jakaya Kikwete aliyoifanya
hivi karibuni, ambapo wako katika maeneo mbalimbali ya Bandari, Reli na yule
atakayesaidia kuanzisha usafiri wa treni kuelekea Gongolamboto ambaye
ametuonyesha aina ya treni inayoweza kutumika katika reli yetu,”alisema Dk
Mwinjaka.
Hata hivyo,
alisema baadhi ya wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo ya
bandari nchini ambapo watapelekwa katika bandari ya Dar es Salaam lakini
kipaumbele ni kwa sasa ni Mtwara.
Dk Mwinjaka,
alisema Mtwara imepewa nafasi kubwa katika uimarishaji wa bandari yake, hiyo inatokana
ugunduzi wa gesi na miradi mingine ya makaa yam awe na chuma chapua ambapo
vyote hivyo vitahiji kusafirishwa kwa haraka kupitia bandari hiyo.
“Wapo
walionesha nia ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Reli ya Kati sasa hawa
tutawaelekeza katika Idara zinazohusika kama vile Rahako,”alisema Dk Mwinjaka.
Akizungumzia
kuhusu ajali zinazotokea, alisema baadhi ya wawekezaji hao wako tayari kuwekeza
katika kuingiza vifaa vya kisasa ambavyo vitaweza kuayagua magari ambayo hayata
kuwa na vigezo vitakavyoruhusu yatembee barabarani kama ilivyo sasa.
No comments:
Post a Comment