HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2015

LOWASSA ATIKISA JIJI LA MWANZA KUSAKA WADHAMINI, POLISI YATAWANYA WAFUASI WAKE KWA MABOMU YA MACHOZI

Umati wa maelfu ya watu ukiwa umekusanyika katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza wakimsikiliza mgombea urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa. Wakati wa mapokezi yake kwenye Uwanja wa Ndege Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi ili kutawanya umati wa watu uliokusanyika nje ya uwanja huo kwa leo la kumpokea mgombea huyo.
Wafuasi wa Ukawa wakiwa katika mkutano wa mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa.
 Msafara wa Lowassa jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na James Lembeli wakiwapungia mikono wanachama na wafuasi wa vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, NLD na Chadema.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa Umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha.
 Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza ukiwa umefurika kwa wingi katika Barabara kuu ya kutoka Uwanja wa Ndege kuelekea katikati ya mji, wakati wa mapokezi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,ambaye yupo kwenye ziara ya kutafuta wadhamini.
 Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa akiwa na mgombea Mwenza, Juma Haji Duni.
 Mbowe akihutubia umati wa watu waliokusanyika katika viwanja vua Furahisha jijini Mwanza.
 Mgombea Urais wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa akipeana mkono na mgombea Mwenza, Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akihutubia Umati wa Wakazi wa Jiji la Mwanza uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Furahisha, wakati wa Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini  na kutambulishwa kwa wananchi, 

No comments:

Post a Comment

Pages