WAZIRI Mkuu wa zamani Frederick
Sumaye, ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kuvumisha kuwa angekutana na vyombo vya habari ili kujivua uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Siku za hivi karibuni tangu
kuhama kwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Eduard Lowassa, kumezuka wimbi
kubwa la baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kujivua uanachama na kuhamia
Chadema.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sumaye, alisema taarifa hiyo ilimshangaza kwa avile
hakuwa na mpango huo.
Alisema hivyo kwa vile
hakuwahi kuzungumza na mtu yeyeto na hajui chochote kuhusu mkutano huo na
vyombo vya habari isitoshe hivi sasa yuko Hanang.
“Mimi watu ambao wameniuliza
nimewambia yani hiyo kitu hata mimi sijui kiukweli wala siko Dar es Salaam.
“Ninasikia kuna mwandishi
ameamua kutupia taarifa hiyo kwenye mambo yenu haya ajabu ajabu, hajazungumza
na mimi wala sijawahi kuzungumza naye wala sina mpango huo,”alisema Sumaye.
Kuhusu kuhamia Chadema,
Sumaye, alisema kama angehamia chama hicho angeviambia vyombo vya habari au angeonekana
akipewa kadi.
“Hivi mimi naweza ni kamahama
kisiri siri kweli ni waambi tu kuwa sina mpango wowote wa kukihama chama
hiki,”alisema Sumaye.
Sumaye, aliwashangaa na
haelewei wanaofanya hivyo wana lengo gani naye, akidai mbona hawaandiki taarifa
za hao wanaohama, wange waandika hao kama wanataka kuandika.
No comments:
Post a Comment