HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 27, 2016

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO

1
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.
Usafiri DART umekuwa mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo. (PICHA NA JOHN BUKUKU)
2
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
3Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
4
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.
6
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
7
Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
10
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
11
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
12
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza.
13
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikaua kituo cha Kimara Mwisho.
14
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David Mwaibula.
8
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu hiyo leo kulia ni Mzee David Mwaibula na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.

No comments:

Post a Comment

Pages