Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

CHOUGHULE: NITACHAPA KAZI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM

Sharik Choughule
NA MWANDISHI WETU
 
MWENYEKITI Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kivukoni, Dar ers Salaam, Sharik Choughule ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa kuenzi juhudi za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli katika ujenzi wa CCM Mpya, Tanzania Mpya.

Amesema, anaamini juhudi zilizoanza kufanywa na Dk. Magufuli zinadhihirisha kwamba zitakifikisha Chama Cha Mapinduzi katika mageuzi ya kweli kukifanya kuwa cha wanachama na kimbilio la wanyonge na pia dhamira ya kuijenga Tanzania mpya ya uchumi wa viwanda itafanikiwa hivyo ni lazima aungwe mkono kwa dhati.

Choughule amesema hayo,  katika salam zake kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kata ya Kivukoni, katikia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki, ambapo salam hizo amezielekeza kwa CCM taifa kwa kuweka mchakato na usimamizi mzuri wa uchaguzi ndani ya Chama.

Amewashukuru pia vuiongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Wilaya ya Ilala na kata hiyo na wanachama kwa ujumla  kwa kuendesha uchaguzi huo vizuri na kwamba ushindi aliopata siyo wake binafsi bali wa wana CCM wote wa kata hiyo, hivyo kilichobaki sasa ni kushikamana na kuijenga CCM mpya yenye kuwajali wanyonge.

Choughule ameahidi kushirikiana na wale aliogombea nao na pia kuhakikisha anashirikiana na wanachama na viongozi wote ili kuifanya CCM katika kata hiyo mbali na kupiga hatua kisiasa lakini pia inapige hatua kiuchumi, kwa kuanzisha miradi ya maendeleo yenye ushirikishwaji wa wanachama wote.

"Kama mnavyojua, CCM katika maeneo mengi imekuwa ikiyumbishwa na kuwa tegemezi, jambo hili si zuri, hivyo moja ya mikakati yangu katika uongozi wangu ni kuhakikisha Chama kinakuwa na miradi ambayo itasaidia kuendesha shughuli za chama badala ya kutegemea wahisani", alisema Choughule.

"Pamoja na kuanzisha miradi lakini nitahakikisha chama kinakuwa imara kwa kuongeza idadi ya wanachama na pia kuchukua nafasi zote za uongozi katika ngazi za serikali za mitaa na udiwani na pia kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha Kivukoni inatoa kura nyingi za kishindo kwa mgombea wa Ubunge na Urais kwa tikteti ya CCM katika Uchaguzi mkuu wa 2020", alisema Choughule .
 MWENYEKITI Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kivukoni, Dar ers Salaam, Sharik Choughule akiwa viongozi wa CCM Kata hiyo na mwakilishi kutoka Wilaya ya Ilala, baada ya uchaguzi kufanyika mwishoni mwa wiki

No comments:

Post a Comment