HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 15, 2017

WANNE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI TANO

NA KENNETH NGELESI, MBEYA

WATU wanne walifariki dunia na wengine tisa kujehuriwa katika ajali ya barabarani iliyuhisisha gari tano katika eneo la Mlima Iwambi,Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya DCP Mohammed R. Mpinga ajali hiyo ilitokea Semptemba14 mwaka huu majira ya saa 19:45 usiku.

Aidha taarifa hiyo ilibainisha magari yanihusika katika ajali hiyo kuwa ni T. 231 BME aina ya Tipper ikiendeshwa na dereva Fred Mwakalinga (33) Mkazi wa Itiji-Mbeya ikitokea Mbeya mjini kwenda Mbalizi.

Gari nyingine ni T. 515 ARE aina ya Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Emmanuel Julius (29) Mkazi wa Itiji ikitokea Mbalizi kwenda Mbeya mjini, na Gari yenye namba za usajili T.126 DJZ aina ya Fuso basi iliyokuwa ikiendeshwa na Amos Mwaikaja (40) Mkazi wa Kagera Soweto jijini Mbeya.

Aidha taarifa ya kamanda inaeleza kuwa gari lingine ni BCA 8730  na tela BCA 8733 lilokuwa likiendeshwa na Evans Musonda (39) raia wa Zambia na Gari yenye namba za usajili T.570 CKC aina ya Toyota dyana ikiendeshwa na dereva Amos Benson pamoja na Pikipiki moja ambayo haijafahamika namba zake za usajili ikiendeshwa na Jania Jackobo Sanga (27) Mkazi wa Iwambi.

Waliofariki katika ajali hiyo ni dereva wa gari yenye namba za usajili T.570 CKC Amos Benson,mwendesha Pikipiki ambayo bado hajafahamika namba zake za usajili aitwaye Jania Jackobo Sanga (27) Mkazi wa Iwambi, dereva wa gari lenye namba za usajili BCA 8730/BCA 8733 Evans Musonda (39) raia wa Zambia na Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika ambaye alikuwa abiria kwenye Gari yenye namba za usajili T.570 CKC Toyota Dyana.

Aidha katika ajali hiyo, watu wengine tisa walijeruhiwa kati yao wanaume ni wanne na wanawake watano kati yao wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na saba wamelazwa Hospitali Teule Ifisi - Mbalizi.

Chanzo cha ajali kinachunguzwa hata hivyo inahisiwa kuwa dereva wa lori alikosa umakini na kuanza kugonga magari mengine ambaye pia amepoteza maisha katika ajali hiyo na kwamba upelelezi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha ajali na dereva aliyehusika.

No comments:

Post a Comment

Pages