NA
KENNETH NGELESI, MBEYA
WATU
wanne walifariki dunia na wengine tisa kujehuriwa katika ajali ya barabarani
iliyuhisisha gari tano katika eneo la Mlima Iwambi,Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa
wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya DCP Mohammed R. Mpinga ajali hiyo ilitokea Semptemba14 mwaka huu
majira ya saa 19:45 usiku.
Aidha
taarifa hiyo ilibainisha magari yanihusika katika ajali hiyo kuwa ni T. 231 BME
aina ya Tipper ikiendeshwa na dereva Fred Mwakalinga (33) Mkazi wa Itiji-Mbeya
ikitokea Mbeya mjini kwenda Mbalizi.
Gari
nyingine ni T. 515 ARE aina ya Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Emmanuel Julius
(29) Mkazi wa Itiji ikitokea Mbalizi kwenda Mbeya mjini, na Gari yenye namba za
usajili T.126 DJZ aina ya Fuso basi iliyokuwa ikiendeshwa na Amos Mwaikaja (40)
Mkazi wa Kagera Soweto jijini Mbeya.
Aidha
taarifa ya kamanda inaeleza kuwa gari lingine ni BCA 8730 na tela BCA 8733 lilokuwa likiendeshwa na Evans
Musonda (39) raia wa Zambia na Gari yenye namba za usajili T.570 CKC aina ya Toyota
dyana ikiendeshwa na dereva Amos Benson pamoja na Pikipiki moja ambayo
haijafahamika namba zake za usajili ikiendeshwa na Jania Jackobo Sanga (27) Mkazi
wa Iwambi.
Waliofariki
katika ajali hiyo ni dereva wa gari yenye namba za usajili T.570 CKC Amos Benson,mwendesha
Pikipiki ambayo bado hajafahamika namba zake za usajili aitwaye Jania Jackobo Sanga
(27) Mkazi wa Iwambi, dereva wa gari lenye namba za usajili BCA 8730/BCA 8733 Evans
Musonda (39) raia wa Zambia na Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika ambaye
alikuwa abiria kwenye Gari yenye namba za usajili T.570 CKC Toyota Dyana.
Aidha
katika ajali hiyo, watu wengine tisa walijeruhiwa kati yao wanaume ni wanne na
wanawake watano kati yao wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na saba wamelazwa
Hospitali Teule Ifisi - Mbalizi.
Chanzo
cha ajali kinachunguzwa hata hivyo inahisiwa kuwa dereva wa lori alikosa
umakini na kuanza kugonga magari mengine ambaye pia amepoteza maisha katika ajali
hiyo na kwamba upelelezi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha ajali na
dereva aliyehusika.
No comments:
Post a Comment