Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Majengo ya DEGE ECO VILLAGE mradi wa ubia kati ya Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF na Azimio wa nyumba 7,4460 zilizopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
*Aagiza wakurugenzi wakuu wa NSSF, AZIMIO, Kamishna TRA wakutane
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi
wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach
Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi
unaendelea kwenye eneo hilo.
Amewaagiza
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya
Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal wakutane na Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane
namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi.
Waziri
Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12,
2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi
ya 7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi
unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.
“Kuna
mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja
kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima
uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la
kuhifadhia vifaa vya ujenzi.”
Kwa upande wakeMkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Erio alimuahidi Waziri Mkuu kwamba atahakikisha
wanakutana na Kamishna wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya AZIMIO
ili kujadiliana na namna ya kuimarisha ulinzi na kutatua changamoto ya
wizi wa mali unaoendelea katika eneo hilo.
Mkataba
kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Limited (AHEL) ulisainiwa mwaka
2012 na kuanzisha kampuni ya hodhi ya “Hifadhi Builders” ambapo AHEL
ilikuwa na asilimia 55 na NSSF asilimia 45. Katika asilimia 55 za AHEL,
asilimia 20 ni ardhi iliyotoa kwenye mradi na asilimia 35 angetakiwa
kuweka fedha taslimu.
Mradi
ulihusisha ujenzi wa nyumba 7,460 ambapo jumla ya gharama za mradi
zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani 653,436,675 ambazo kati yake ujenzi
ungegharimu Dola 544,530,562 wakati gharama za ardhi zingekuwa Dola
108,906,113. Kwa fedha za Tanzania mradi pamoja na ardhi ungegharimu sh.
trilioni 1.5.
Hadi
kufikia Juni 2018 NSSF walishailipa kampuni ya Hifadhi Builders Dola
133,838,662.2 kama mchango wake kwenye ujenzi wa mradi huo ambazo ni
sawa na sh. bilioni 305.8 wakati kampuni ya Azimio ikitoa Dola 5,500,000
sawa na sh. Bilioni 12.6 tu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, NOVEMBA 13, 2018.
No comments:
Post a Comment