HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 12, 2019

RAIS WA ZANZIBAR MHE. DK. SHEIN APOKEA GWARIDE LA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR UWANJA WA GOMBANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapungua Mkono Wananchi akiwa katika gari Maalum ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, wakati akiingia katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, akiwa Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, Brigedia Jenerali Fadhil Omar Nondo. (Picha zote na Ikulu)
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, wakionesha jinsi ya uchezaji wa Gwarige la kimya, wakati wa Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wananchi wakati wa sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
 Mke wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume, Mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Mama Anna Mkapa na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mama Shadya Karume, wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.
Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wakionesha jinsi ya uchezaji wa gwaride la zamani, wakati wa sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani.
Askari wa Kikosi cha KMKM wakitoa heshima wakiwa katika mwendo wa kasi wakati wa maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika Uwanja wa Gombani Pemba.
Kikosi cha Makomandoo wa JWTZ wakipita kwa ukakamavu wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Uwanja wa Gombani Pemba.

No comments:

Post a Comment

Pages