Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Nataka kulewa’, Msanii
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ ameachia
kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Kesho’ ikiwa ni muendelezo wa
kutoa burudani kwa mashabiki wake.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam leo, Diamond
amesema ngoma hiyo kaipeleka sokoni juzi na kwamba yupo katika mchakato wa kutengeneza
video ya kazi hiyo ambayo anaimani itakuwa na ujumbe mzito katika jamii.
“Naimani kazi hii itafanya vizuri, nimeamua kuachia kazi
zangu mfululizo kwa madai ya baadhi ya mashabiki kwamba nimeishiwa mistari,
kazi nyingine naachia baada ya Christimas huu utakua wimbo wa kuuga mwaka na
kuukaribisha mwaka mwingine,” anasema Diamond.
Anasema yeye hawezi kuishiwa mistari kirahisi kama
wanavyomfikiria wanaoongea, anawaomba mashabiki wa kazi zake waendelee kumpa
sapoti katika kazi zake na kuwataka wasicheze mbali nay eye kuna vitu vingi
ambavyo amewaandalia.
Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Diamond alishawahi
kutamba na vibao vyake kama, Mbagara, Mawazo, Moyo wangu na nyingionezo ambazo
zilimuweka pazuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.
No comments:
Post a Comment