HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 10, 2012

ROBERTO MANCINI AWABWATUKIA NYOTA MANCHESTER CITY


 Ashley Young na Robin van Persie wakishangilia bao la Wayne Rooney katikati, wakati Man United ilipowalaza Man City mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Etihad.
 Mario Balotelli katikati, akizuiwa asipambane na mashabiki wakati wa pambano la mahasimu wa jiji la Manchester, lililoisha kwa City kulala nyumbani Etihad kwa mabao 3-2 mbele ya wageni wao Man United.
 Robin van Persie akishangilia bao lake la 'usiku' kuipa ushindi wa 3-2 Man United dhidi ya Man City.
 Huyu ni shabiki wa Man City akizuiwa na mlinda mlango Joe Hart asiende kumpiga beni wa Man United Rio Ferdinand aliyeenda kushangilia upande wao baada ya RVP kufunga bao la ushindi. Ferdinand alipigwa kitu chenye ncha kali na kukatwa juu ya jicho lake na mashabiki hao.
Hapa ilikuwa mapema wakati Wayne Rooney alipoifungia United moja ya mabao yake katika mtanange huo. 

MANCHESTER, England

Bila kuuma maneno, Mancini ‘akamchana live’ mlinda mlango wake Joe Hart na kumwambia, “Yalikuwa ni makosa yako” yaliyoruhusu uvunjifu wa rekodi ya kutofungwa msimu huu kwa Man City katika Ligi Kuu

ROBERTO Mancini aligeuka mbogo kwenye vyumba vya kuvalia vya Manchester City, baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kuruhusu bao la mwishoni la adhabu ndogo la Robin van Persie kuwanyima sare katika pambano la mahasimu dhidi ya Manchester United.

Bila kung’ata maneno, Mancini ‘akamchana live’ mlinda mlango wake Joe Hart na kumwambia, “Yalikuwa ni makosa yako” yaliyoruhusu uvunjifu wa rekodi ya kutofungwa msimu huu kwa Man City katika Ligi Kuu ya England.

Baada ya kumlaumu waziwazi Hart, bosi huyo wa City akawageukia wakali wake Mario Balotelli, Carlos Tevez na Samir Nasri.

Balotelli alisangaza wengi kupangwa kikosi cha kwanza, kabla ya kutolewa mapema kumpisha Tevez. Ndani ya vumba vya kuvalia, akasikika akisema: “Mancini amechanganyikiwa, inaonekana anataka mapambano na na kila mmoja.”

Mancini pia alikasirishwa na jitihada hasi za Tevez na Nasri katika kuyepuka kile Van Persie alichofanya mwishoni mwa mtanange huo wa kukata na shoka.

Tevez alisababisha adhabu ndogo, ambayo wakati ikipigwa aliondoka na kushindwa kujipanga kwenye ukuta kuizuia na Mancini alisema: “Sijui kwanini. Najua kabla ya kupigwa adhabu ile ilikuwa hatari, sijui ni kwa nini ilitokea.

“Mchezaji wa kupiga adhabu ile alikuwa ni Van Persie na aliipiga vema. nilimuita sana Carlos arudi kwenye ukuta kuzuia, lakini bahati mbaya nilikuwa mbali mno kwenye benchi.”

Kwa upande wake Nasri alizuia vibaya adhabu hiyo kea kukaa nyuma ya Edin Dzeko,kisha akaugusa mpura wa RVP na kumpoteza maboya kipa wake Hart.

Mancini akaonngeza: “Tulifanya makosa na kimsingi kulikuwa na wachezaji watatu tu kwenye ukuta wa kuzuia. Ni kama tulikuwa na wachezaji wawili na nusu katika ukuta huo, hakuzuia vema kabisa.

“Nadhani ukuta unapaswa kuwa bora. Nafikiri katika sekunde za mwisho tulipaswa kuwa na zaidi ya umakini katika hali hiyo. Kama unahitaji kuweka uso wako huko, unapaswa kuweka uso wako.”

Man City walionekana kupoteana katika dakika za awali za pambano hilo ndani ya dimba la nyumbani la Etihad na kumruhusu Wayne Rooney kufunga mara mbili, kabla ya Mancini kumtoa Balotelli na kumwingiza  Tevez.

No comments:

Post a Comment

Pages