HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 10, 2012

LIONEL MESSI AVUNJA REKODI YA MABAO YA GERD MULLER


 Nahodha wa Barcelona, Carles Puyol kulia, akimpongeza Lionel Messi kushoto baada ya kufunga bao dhidi ya Real Betis. Katikati ni kiungo Andres Iniesta wa klabu hiyo. Barcelona ilishinda 2-1.
 Messi hapa akishangilia uvunjaji rekodi ya mabao ya Gerd Muller ya mabao 85 iliyodumu kwa miaka 40.
Hapa Mess akichuana na mabeki wa Betis katika mtanange huo.

BARCELONA, Hispania

Kati ya mabao 86 aliyofunga Lionel Messi kwa kalenda ya mwaka huu wa 2012, mabao 74 ameifungia klabu yake ya FC Barcelona, huku mengine 12 akiifungia Argentina katika jumla ya mechi 66 za klabu na timu ya taifa

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona na mshindi tatu mfululizo za Mchezaji Bora wa Mwaka Lionel Messi, jana usiku amevunja rekodi ya muda mrefu ya upachikaji mabao kwa kufunga mabao 86 kwa mwaka huu wa 2012.

Messi, 25 ambaye nia nyota wa kimataifa wa Argentina, ameivunja rekodi ya Gerd Mueller ya kufunga mabao 85 mwaka 1972 – na kuweka rekodi mpua ya utikisaji nyavu ngazi ya klabu na timu ya taifa.

Nyota huyo anayewania tuzo ya nne ya Balon d’Or, aliivunja rekodi ya Mjerumani Muller, kwa kufunga mara mbili na kuipa Barca ushindi wa 2-1 dhidi ya Real Betis katika mechi kali ya La Liga iliyopigwa Jumapili.

Akiwa na mabao 84, Messi alifunga bao la kwanza lililomfanya amfikie Muller (mabao 85) kunako dakika ya 16 ya pambano hilo, kabla ya kufunga la pili lililomfanya aweke rekodi mpya (mabao 86) katika dakika ya 25.

Awali ilionekana kama Messi angeshindwa kuifikia ama kuivunja rekodi ya Mueller mwaka huu, baada ya kukamiwa na mabeki wa Benfica katika mechi ya Mabingwa Ulaya, aliyoumia na kutolewa.

Nyota huyo akaingia shakani kuvunja na kuweka rekodi, akiamini alipata jeraha ambalo lingemchukua muda kurudi dimbani, ingawa ilikuja kugundulika hakuumia sana na kumfanya aanze kikosini juzi.

Kati ya mabao 86 aliyofunga Messi kwa kalenda ya mwaka huu wa 2012, mabao 74 ameifungia klabu yake ya FC Barcelona, huku mengine 12 akiifungia Argentina katika jumla ya mechi 66 za klabu na timu ya taifa.

Hata hivyo ana nafasi ya kuongeza idadi ya mabao kabla ya kumalizika kwa mwaka huu, kwani kabla ya mwaka mpya Barcelona itacheza mechi tatu – zikiwamo mbili za Ligi Kuu na moja ya Kombe la Mflame.

"Daima nimekuwa nikisema sawa na nilichowahi kusema, ni nzuri kwamaana, lakini yshindi wa timu ndio muhimu zaidi hasa ukizingatia unatufanya tuwaongoze wengine," Messi alisema kuiambia Canal Plus baada ya mechi.

"Lengo langu wakati mwaka ukianza ilikuwa ni kupata mafanikio tena kadri niwezavyo, hikiwa na timu yangu katika Ligi Kuu, Kombr la Mfalme na Ligi ya Mabingwa Ulaya."

Enzi zake, Mueller alifunga jumla ya mabao 72 akiwa na klabu yake ya Bayern Munich, huku akitikisa nyavu mara 13 akiwa na timu ya taifa ya iliyokuwa Ujerumani Magharibi katika mwaka wa 1972.

Akizungumza baada ya mechi na rekodi hiyo ya Messi, kocha wa Barca Tito Vilanova alisema: “Rekodi ya Leo ni ya kuvutia sana. Ni ya kupendeza wakati unapofikiria kwamba yeye sasa amefunga mabao mengi mno.

"Baadhi ya wachezaji ufunga uidadi hii ya mabao kwa miaka kati ya saba au nane, yeye amefunga ndani ya mwaka mmoja. Na mengi kati ya mabao hayo ni bora na mazuri sana,” alimaliza Vilanova.

1 comment:

  1. Write more, thats all I have to say. Literally, it seems as though you relied on the video to make your
    point. You definitely know what youre talking about, why throw away your intelligence on just posting videos
    to your weblog when you could be giving us something enlightening to read?
    Here is my blog ... BCN box

    ReplyDelete

Pages